JAMANI NIPE CHANCE KIDOGO 14&15* "Abisai kwanini unakuwa sio muelewa, Erick ni rafiki yangu wa kawaida tu, kwani wewe haujawahi kuwa na marafiki wakike?

Niliacha nao siku nyingi baada ya kuona hawana maana kwenye maisha yangu. Na hata wale niliowabakiza niliamua kuachana nao kabisa baada ya kupata wewe mwanamke ambae tunaendana. Leyna hivi umeshawahi kujiuliza pamoja na mambo yako ya kuvunja moyo na kukatisha tamaa lakini bado nilikuwa sikati tamaa ya kuwa na wewe? Leyna alimuangalia bila kusema chochote. "Kama ulikuwa hujui basi leo nakwambia. Sababu nakupenda Leyna, baada ya kuteseka sana kwenye mahusiano yangu huko nyuma sikutamani kupenda tena. Hata nilipo ondoka na wewe pale club ilikuwa napitia tu baada ya hapo naendelea na mambo yangu lakini upendo wangu ukanifanya niwe king'ang'anizi kwako.

Soma zaidi