MIMBA YA DHARURA* *_____________________________________*  *SEHEMU YA KUMI NA MOJA*

Nadia alibaki amekaa kwenye kiti chake, akili yake ikimzunguka kama upepo mkali. Kila jambo lililokuwa likitokea maishani mwake lilionekana kama sinema ya ajabu. “Jayden anataka kuwa baba wa mtoto wangu?” alijiuliza taratibu huku akijiegemeza nyuma ya kiti. Machozi yalijaa machoni kwake sio kwa sababu ya huzuni , bali kwa mshangao na mchanganyiko wa hisia. Hakuwahi ameota ndoto kwamba siku moja mwanaume mwingine angejitokeza kwa ujasiri kiasi hicho, akitamani kumchukua yeye na mtoto wake kama sehemu ya maisha yake. Lakini bado kaburi la maumivu ya Kabir na kumbukumbu za usaliti wa Jawad halikuwa limefukiwa. Usiku Nadia alikaa kitandani akimwangalia Tawakal aliyekuwa

Soma zaidi