𝗖𝗘𝗢 𝗡𝗔 𝗠𝗥𝗘𝗠𝗕𝗢 𝗪𝗔 𝗧𝗜𝗞𝗧𝗢𝗞 SEHEMU YA 16 ENDELEA..... "Ni wakati wa wewe kufurahia uboss pia, sielewi ni kwanini unapoteza kujiamini ✋" Zara aliongea.

"Hujanijibu swali langu, Bryant Kobe ameniachia kiti kwa hiari yake au umemuomba?" "Bila kumuomba unadhani angeachia nafasi kwa hiari yake, unajua siku zote huwa unaamini Bryant Kobe anakupenda lakini upendo wake ni wa kinafiki.... tabasamu analo kuonyeshaga huwa ni danganya toto tu ili usije kwenda kinyume naye ....ni wakati wa wewe kuitwa boss pia. Kila Mama ana tamaa ya kumuona mtoto wake matawi ya juu. Naomba sana usije kukuza maneno utaniumiza moyo wangu " Zara alijihami kwa kuporomosha machozi. "Hapana, kuna kitu utakuwa umemuambia Bryant Kobe ana tabia ya kukusikiliza kwa kila kitu, acha kudondosha machozi yako kwa sababu sitakubembeleza

Soma zaidi