NILIZAA NA BOSI KWA BAHATI MBAYA SEHEMU YA 04

TULIPOISHIA ....... Bosi alikuwa anataka kusema kitu. Niliona midomo yake ikifunguka taratibu, macho yake yakinitazama kwa umakini wa ajabu, kana kwamba alikuwa anapima uzito wa neno alilotaka kulitamka. Lakini kabla hajazungumza ANZA NAYO SASA...... GHAFLA Simu yake Ikaanza kuita ... Sauti ile ilikatiza kila kitu. Alishtuka kama mtu aliyerudishwa ghafla duniani. Akavuta mkono wake haraka, akasimama, na kuchukua simu ile huku akigeuka pembeni. “Hello?” alisema kwa sauti iliyobadilika kabisa, sauti ya bosi niliyoizoea. Mimi nilikaa pale kitandani, moyo wangu ukipiga kwa nguvu. Nilikuwa najilaumu, na wakati huohuo nikishindwa kuelewa nilichokuwa nakihisi. Ni hofu? Ni aibu? Au ni kitu kingine ambacho

Soma zaidi