
Nilishtuka ghafla. Nilikuwa nimelala juu ya kitanda kikubwa, cheupe, chenye harufu ya manukato ya kiume. Pazia la dirisha lilikuwa likiruhusu mwanga wa asubuhi uingie taratibu, na saa ya ukutani ilionyesha saa kumi na moja alfajiri. Moyo wangu ulianza kupiga kwa kasi. "Nimefikaje hapa?" "Hii siyo ofisi." "Hiki ni kitanda cha nani?" Nilijaribu kukumbuka. Kichwa kilikuwa kizito, mwili umechoka lakini hakuna maumivu. Niliangalia nguo zangu nilikuwa bado nimevaa vizuri, japokuwa suti ilikuwa imelegea kidogo kana kwamba nililala nayo. Nilinyanyuka taratibu, nikakaa kitandani huku nikishika kichwa changu. Ndipo mlango ukafunguliwa. Aliingia bosi wangu Mr. Adrian. Alikuwa amevaa shati jeupe, mikono imekunjwa, uso
0 Comments