๐ฉ๐๐ง๐๐๐จ ๐ฉ๐๐ก๐๐ฉ๐ฌ๐ข๐๐๐๐๐๐๐ฆ๐๐ ๐ ๐๐๐ฆ๐๐ (๐ฉ๐ฉ๐ ) ๐ฉ๐ถ๐น๐ถ๐๐๐ผ๐ฎ๐ป๐ฑ๐ถ๐ธ๐๐ฎ ๐ก๐ฎ: ๐๐ฆ๐๐ข๐๐จ ๐ ๐๐จ๐จ ๐ญ๐๐๐๐๐ฅ๐ฌ ๐๐๐๐ข๐๐ Napenda kuchukua nafasi hii, kuwashukuru wanamaombi wote, kokote mlipo; ambao mmekuwa mkiiombea kazi hii ya Uandishi wa Vitabu; ambayo nimekuwa nikiifanya kwa muda sasa. Maombi yenu yameifanya kazi hii kubwa, kuendelea kwa ufanisi mkubwa, kwani kama wengi wetu tunavyofahamu; kazi hii isingewezekana kamwe kufanyika, pasipo maombi (YAKOBO 4:2; UFUNUO WA YOHANA 8:3-5). Zaidi sana, ninamshukuru Roho Mtakatifu, ambaye amekuwa akitufundisha njia itupasayo kuiendea, katika kuifanya kazi hii; na kutushauri, jicho lake likitutazama (ZABURI 32:8); na kuvifanya Vitabu hivi, kuandikwa kwa uvuvio wake; na uwezo wake wa kipekee (YOHANA 20:22; ZEKARIA 4:6; LUKA 24:49). Baada ya Shukurani hizi, nimeona vema pia, kuwapa ninyi wanamaombi mnaoiombea kazi hii; na pia kuwapa umma wote, kwa ujumla wake; mrejesho kuhusu maendeleo ya kazi hii ya Uandish