STORY PENZI LA MTEKAJI 1 & 2

Story......... PENZI LA MTEKAJI 1......2 Mkasa...wa...kusisimua Sehemu Ya {01} Yapata kama majira ya saa sita mchana, hali ya hewa ilikuwa ya mawingu kuashiria mvua inataka kushuka, jua lilifichwa na mawingu mazito yaliyosindikizwa na upepo mwanana uliomfanya kila mmoja afurahie maana ulikuwa ukivuma taratibu sana. Wakati hali hiyo inaendelea katika ofisi moja ya kampuni ambayo inajishughulisha na maswala ya fashion walionekana mabinti watatu wameketi wakizungumza na mabinti hao walikuwa ni watu wa karibu sana. Walikuwa wakiongea mengi sana lakini kubwa zaidi waligusia swala la mahusiano na kila mmoja alikuwa akisifia mahusiano yake lakini binti mmoja alikuwa kimya na ndie aliekuwa bosi wa kampuni hiyo. Huenda ikawa hana mpenzi au mapenzi yake yalikuwa na mgogoro hilo halikujulikana lakini alionekana kuwa kimya akiwatazama wenzake. "Lakini Suzana we nawe umezidi bosi yaani kila mwanaume anaekutokea na kukutongoza unamkataa sasa sijui unahitaji mwanaume wa aina gani jamani.!!" Alizungumza mwanamke mmoja mweupe mnene ambae nae alikuwa ni miongoni mwa wanawake hao. "Hebu Sabina muache bhana huenda anataka kuja kuolewa na Rais" "Sasa Raisi gani tena wakati Raisi wetu mama Samia ni wa kike au anataka kuja kuolewa na Hussein Mwinyi Raisi wa Zanzibar.!!" Basi yalikuwa ni maongezi yaliyojaa utani lakini Suzana alikuwa kimya akiwasikiliza na pia hakuwa muongeaji sana alibaki kuwatazama wenzake waliozidi kumsema.. "Jamani kama mmemaliza kunisema haya tokeni muende kuendelea na majukumu yenu maana mnaona humu kama sehemu ya kuongea umbea haya inukeni na mtoke" Suzana alikuwa amechukia kiasi chake na hakutaka kuendelea kusikiliza maongezi yao hivyo aliona awafukuze ili kuondoa kero. Basi wale mabinti yaani Sabina na mwenzake Sheila ilibidi wainuke na kuondoka zao wakimuacha Suzana kwenye mawazo mengi, haelewi aanze wapi aishie wapi. "Lakini wanachosema wenzangu ni kweli naweza kuzeeka bila kupata mpenzi sasa acha nitafute mh hapana siwezi kutafuta nikaonekana mwanamke rahisi najua nitafuatwa tu" Suzana baada ya kubaki mwenyewe aliyawaza hayo na mwisho alichukua peni pamoja na karatasi kisha alitoka nje kwenda kuangalia maendeleo ya vijana wake aliowaajiri kama wanafanya kazi kwa ufasaha. Suzana alikuwa ni binti wa miaka 23 binti aliekuwa na pesa nyingi sana ambazo amezirithi kutoka kwa wazazi wake, pia Suzana alikuwa akiishi na mama yake mkubwa ambae ndie amemlea tangu wazazi kufariki mpaka anakuwa na kujielewa. Kingine Suzana alikuwa ni binti mkimya asiependa mazoea ovyo na hiyo ndio ilipelekea mpaka wakati huo kuishi bila mpenzi na mama yake mkubwa alikuwa akimsisitiza kila siku kutafuta mwenza lakini alipotezea. Basi tutoke huko sasa kwa Suzana tuje upande wa pili ambapo huku alionekana kuna kijana wa makamo akiwa chumbani kwake katika nyumba ya kupanga na kulikuwa ni uswahilini hivyo kelele za watoto zilisikika nnje ya chumba chake. Kelele hizo za watoto hazikumfanya kushindwa kufanya kazi yake na wakati huo alikuwa busy kusafisha bastola yake ambayo hiyo huitumia muda mwingi katika majukumu yake. Kijana huyo alifahamika kwa jina la Novan na alikuwa kijana mpole, aliependa jamii inayo mzunguka lakini licha ya upole wake ila alikuwa ni kijana anaetumiwa kihalifu hasa katika mambo ya utakaji na uuwaji. Wakati yupo busy kusafisha bastola yake mara simu yake ilianza kuita hivyo aliichukua na kupokea kisha aliweka sikioni. "Hey Novan unahitajika na bosi usiku wa leo kwahiyo ifikapo majira ya saa mbili uwe hapa kuna jukumu linawahusu hapa" "Ok sawa haina shida" Baada ya simu hiyo kukatwa aliweka simu yake kando na kuendelea na zoezi lake la kusafisha bastola, hakuwa na papara wala wasiwasi. Novan alikuwa ni kijana wa miaka 24, kijana mpole na asiependa kuongea sana lakini upole wake ulificha uhalisia wake machoni mwa watu, alikuwa ni kijana mbaya sana ambae kuuwa kwake ilikuwa kama starehe. ***************** Muda ulikwenda, ilipotimu majira ya saa moja usiku Novan alijiandaa vyema kwa kuvalia mavazi yake meusi, alipachika bastola yake kiunoni na kutoa pikipiki yake kubwa ya kisasa ambayo muda mwingi huitumia katika safari zake. Alijipakia na kuanza safari kuelekea makao makuu yao lakini hakujua ni kazi gani ambayo wanakwenda kufanya siku hiyo, either ya utekaji au ya mauaji. Kutokana na kasi ya pikipiki yake alitumia takribani dakika thelathini kufika katika supermarket moja ambayo alipaki pikipiki yake nnje na kushuka, alitazama kushoto na kulia kisha aliingia kwenye supermarket hiyo. Ilikuwa ni supermarket kubwa ambayo hujihusisha na uuzaji wa bidhaa mbali mbali lakini ndani ya supermarket hiyo kulikuwa na mlango wa siri ambao Novan aliingia na kutokea chini ya supermarket ambapo huko ndipo shughuli na mipango yao hufanyika. Alifika na kupokelewa vizuri maana walikuwa wakiijua kazi yake, akipewa jukumu alitimize basi kufeli kwake ni mara chache sana lakini mara nyingi lazima afanya kazi kwa ufasaha na kuikamilisha. "Nafurahi umefika kwa wakati Novan, sasa leo hatuna mission ya utekaji wa mabinti ila leo mtakwenda kwenye club ya santiago ambapo Mr Moses leo anakutaka na tajiri kutoka uturuki kwahiyo nahitaji mumuangamize" Alizungumza bosi au mkuu ambae ndie anawapa mission za kufanya. "Lakini mkuu unajua jinsi gani Mr Moses alivyo na ulinzi sasa huoni kama itakuwa ni ngumu kwetu halafu umetuchagua sisi wawili tu.!?" "Usijali Nason nimewachagua kwasababu nawaamini kwahiyo kwa kushirikiana wewe na Novan naamini mtamaliza jukumu hili na leo nitawapa pesa nzuri endapo mtamuuwa Mr Moses" "Ok sawa" Ilibidi Nason na Novan watoke hapo na kuanza safari kuelekea santiago club ambapo huko ndipo walipangiwa mission. Walitumia usafiri wa gari yao binafsi lakini wakiwa ndani ya gari story pia zilichukua nafasi yake. "Hivi Novan unajua hii kazi nafanya basi tu lakini natamani leo kesho niache maana tunafanya kazi ngumu lakini malipo kidogo, haturuhusiwi kuwa na wapenzi sasa si kama jela tu.!?" "Yah lakini si unajua sheria, kama utajihusisha kimapenzi na mwanamke halafu ukagundulika kinachofuata ni kifo wewe na mtu wako, kwahiyo kaa kwa kutulia mtu wangu tufanye majuku yetu" Novan ilibidi amkumbushe tu Nason huku safari ikichana mawimbi ya barabara kuitafuta santiago club ambayo ilikuwa nnje kidogo ya mji. Wakati safari yao inaendelea huku kwa Suzana alifuatwa na rafiki zake usiku huo na walikuwa wamevalia vizuri kuashiria kuna sehemu walikuwa wanaenda. "Sasa jamani ndio kunifuata usiku nyumbani nataka kulala halafu mbona mmependeza kiasi hicho kulikoni tena.!?" Suzana alibaki kuwatazama wenzake na kuwauliza maana ilionesha walikuwa na safari. "We nae jamani mara hii umesahau wakati tulipanga kwenda santiago club halafu nimepata taarifa kuna band nyingi zitakuwepo, shisha za kumwaga kwahiyo tusichelewe dada fanya haraka twende" "Aaah halafu nilikuwa nimesahau kabisa ok basi sawa nisubiri nijiandae halafu tuelekee huko maana bado muda unaruhusu" Suzana haraka alirudi ndani na bahati nzuri mama yake mkubwa alikuwa amesafiri muda mrefu sana hivyo ikawa kwake huru kufanya chochote. Takribani dakika kumi na tano alizitumia kujiandaa, alipomaliza haraka alitoka na safari ilianza kuelekea santiago club ambapo huko huko Nason na Novan walikuwa wanaenda kufanya jukumu lao la kumuuwa Mr Moses. ******************* Club ilikuwa imefurika, watu kutoka sehemu mbali mbali ya jiji walifika hapo na katika umati huo ndani yake walikuwa marafiki watatu yaani Suzana, Sabina na Sheila, walikuwa wakiangaza huku na kule kutafuta meza nzuri ambayo wangeketi na kupata vinywaji. "Jamani hebu twendeni kuketi kwenye meza ile" Baada ya kuona meza wote kwa pamoja walisogea na kuketi lakini sehemu waliyokaa wao ilikuwa karibu kabisa na sehemu ambayo maongezi ya Mr Moses na tajiri kutoka uturuki yalikuwa yanaendelea na jambo kubwa walikuwa wakiongea kuhusu biashara. Walikuwa hawana ili wala lile na muda huo huo Nason na Novan walifika kama wateja, walitafuta meza na kuketi kisha waliagiza vinywaji ambavyo hawakuvitumia ila waliweka kama urembo huku wakimsomea ramani Mr Moses. Masikioni mwao walikuwa na vibluetooth vidogo ambavyo waliweza kuongea na mkuu wao akiwapa maelekezo nini cha kufanya. "Mkuu tayari tumemuona Mr Moses ila hana ulinzi mkubwa ana vijana wawili tu waliomsimamia pembeni" "Basi muuweni mara moja ila huyo mturuki mumuache maana bosi anamuhitaji kufanya nae biashara, hapo cha kufanya ua huyo Mr Moses ambae ndie kikwazo cha biashara" "Ok sawa" Baada ya mawasiliano hayo Novan na Nason hawakuchelewa walificha nyuso zao kwa mask kisha walipeana signal na kuanza kuwashambulia wale walinzi ili kupata nafasi ya kumuuwa Mr Moses. Risasi mbili zilisikika zilizowaangusha wale walinzi wa Mr Moses chini lakini milio ya risasi hiyo iliwafanya watu kutaharuki na kuanza kukimbia ovyo kutafuta njia ya kutokea humo. Upande wa Mr Moses alijua tayari amekuja kuuwawa maana muda mwingi alikuwa akiwindwa hivyo aliona njia ya kutoka hapo salama ni kumchukua mtu kama ngao ili aweze kukimbia. Alimsogelea kijana wake mmoja aliekuwa chini kisha alichukua bastola na kumvamia binti mmoja aliepita mbele yake ili kumfanya kama ngao na bahati mbaya alikuwa amempata alikua ni Suzana ambae alijikuta akipiga kelele kuomba aachiwe. "We binti tulia mimi siwezi kukuuwa ila nitakufanya kama ngao sasa kama ukileta ubishi nitabomoa kichwa chako" Suzana ilibidi awe mpole kuhofia kufa lakini Nason na Novan walipoona Mr Moses amemtumia mtu kama ngao ilibidi wasogee kwa kujiamini maana walijua hatoweza kufanya chochote. "We mzee hebu acha ujinga sasa unafikiri tukiamua kukuuwa tunashindwa, yaani tunakuuwa wewe na huyo mwanamke kwahiyo muachie huyo binti aende sisi tunataka tudeal na wewe tu" Novan alizungumza huku akisogea zaidi na kumfanya Mr Moses aanze kutetemeka kwa hofu huku kwa Suzana alihisi haja kubwa kumtoka maana mdomo wa bastola ulikuwa kichwani kwake. "Na...nase...nasema asisogee mtu nitaua naombeni mkae mbali, kwanza vueni hizo mask niwaone sura zenu ni wakina nani nyie...!! "Haina haja ya kuvua wewe tunaomba muachie huyo binti aende halafu tutakuacha salama ila kinyume na hapo utakufa" "Sasa nitamshoot risasi kama hamtafanya ninachowaambia" "Ok sawa kuwa mtulivu tutatoa hizi mask lakini umuachie huyo binti" Novan licha ya kuwa muuwaji na mtekaji lakini hakupenda kuona watu wasio na hatia wakifa hivyo ilibidi akubali kuvua mask na kupelekea sura yake kuonekana. "Sasa Novan umefanya nini.!?" "Tulia Nason huyu mzee mbona tutamuuwa wala usijali kwahiyo hapa namzuga tu halafu wewe kaa tayari kumshoot" Mr Moses hakujua kama mipango ilikuwa inapangwa kwa siri, baada ya kuona sura ya Novan alimsukuma Suzana kuelekea alipo Novan kisha alifyatua risasi mbili zilizokuwa zikienda kumpiga Suzana mgongoni lakini Novan aliwahi, alimgeuza Suzana na zile risasi mbili zilipiga mgongoni kwake huku Nason alipata nafasi ya kumshambulia Mr Moses na kumuua.... ITAENDELEA... Story......... PENZI LA MTEKAJI Mkasa...wa...kusisimua Sehemu Ya {02} ILIPOISHIA...... Mr Moses hakujua kama mipango ilikuwa inapangwa kwa siri, baada ya kuona sura ya Novan alimsukuma Suzana kuelekea alipo Novan kisha alifyatua risasi mbili zilizokuwa zikienda kumpiga Suzana mgongoni lakini Novan aliwahi, alimgeuza Suzana na zile risasi mbili zilipiga mgongoni kwake huku Nason alipata nafasi ya kumshambulia Mr Moses na kumuua. ENDELEA NAYO..... Novan alikuwa chini akigugumia kwa maumivu huku damu nyingi sana zikimtoka mgongoni kwake pia upande wa Suzana alikuwa bado mwenye hofu maana alikuwa amenusurika kwenye tundu la sindano pia asingekuwa Novan kukinga risasi basi muda huo angekuwa yeye ndiye anaugulia maumivu ya risasi. "Ka...kaka yangu unaendelaje.!!?" Suzana alisogea mpaka alipo Novan na kumuuliza lakini hakujibiwa kitu, Novan alichukua mask yake na kuirudisha usoni. Wakati huo huo Nason alimchukua na kuondoka nae hawakutaka kabisa kuongea chochote na Suzana walimuacha akiwa mwenye maswali mengi na kujiuliza wale walikuwa ni watu wa aina gani lakini hakupata jibu la kuridhisha akili yake. Wakati Novan na Nason wanaondoka huku nyuma jeshi la polisi likifika baada ya kupata taarifa za uvamizi kwenye club ila walifika na kukuta mashambulizi yamefanyika na kilichobaki ni damu na maiti ya Mr Moses tu. Walitazama pembeni walimuona Suzana ameketi huku akitetemeka kwa hofu, ilibidi wamfuate na kuanza kumuhoji inawezekana wakapata chochote kutoka kwake na wakawajua wahalifu kwa ufupi. "Samahani dada kwanza pole sana kwa kilichotokea hapa najua akili yako haiko sawa kwa sasa lakini nahitaji kujua mawili matatu kwa kilichotokea hapa.?" Askari mmoja wa kike alimfuata Suzana na kuanza kumuuliza maswali lakini Suzana alikuwa mzito kujibu na hata mdomo wake kuufungua aliona kama umefungwa vyuma. "Dada hebu jitahidi japo utueleze machache kuhusu tukio lililotokea hapa lakini ukikaa kimya tutashindwa kufahamu tuanzie wapi tuishie wapi" "Mi...mimi sijui chochote lakini watu waliovaa mask usoni mwao ndio wamefanya hivi lakini kingine sifahamu" "Ok sawa aina shida cctv camera zipo tutaangalia kwahiyo tunaomba uende nyumbani ukapumzike ili akili ikae sawa acha sisi tufanye kazi yetu" Askari ilibidi wamruhusu Suzana kuondoka lakini hata tembea yake ilikuwa kama mtoto mdogo anaejifunza kutembea, basi alitoka mpaka nnje na bahati nzuri kwenye club hiyo kulikuwa na tax nyingi za usafiri zimepaki nnje hivyo aliingia kwenye tax moja wapo na kuomba apelekwe kwake. Wakati hayo yanaendelea Nason alimfikisha Novan kwake na kuanza kumfanyia huduma ya kwanza, alikuwa akimtoa risasi mgongoni pasi na ganzi kisha alimfunga vizuri bandage na kuanza kupiga story zao. "Yaani Novan sasa ulifanya nini pale kumtetea yule binti, mimi nilijua labda utampiga risasi pamoja na Mr Moses na baada yake wewe ndiye umepigwa risasi.!" "Ah sikutaka yule binti afe halafu sisi hatuui watu ovyo ila tunauwa waliokuwa katika target yetu kwahiyo nikaona nimsaidie ila kikubwa mission passed tunatakiwa tukapeleke majibu makao makuu" "Ok sawa haina shida" Novan na Nason walichukuzana hapo na kuelekea makao makuu yao ambapo huko walipokelewa vizuri na taarifa zile zilimfurahisha sana bosi. "Vijana mmefanya kazi kwa weledi mkubwa sana japo kuna makosa mmefanya lakini siku nyingine mabinti kama wale mnaua hakuna kutetea maana unaweza ukajikuta unakufa wewe" "Ok sawa mkuu" Siku hiyo ilifanyika part kwa wahalifu hao lakini Novan hakuweza kuhudhuria maana alikuwa na maumivu makali sana mgongoni hivyo aliomba ruhusu na kurudi kwake kupumzika. Wakati yeye amepumzika kwake na huku Suzana alikuwa amefika kwake muda sana lakini alifikia kupanda kitandani bila kuoga na kuutafuta usingizi ambao ulipeperushwa na mawazo ya tukio lilotokea masaa machache nyuma. "Lakini yule kaka kwanini amenisaidia mimi wakati mimi najua wahalifu hawajali hata mtu akifa kikubwa watimize jukumu lao.!?" "Ila sifikirii kama wahalifu wote watakuwa na roho mbaya, wapo wazuri kama yule kaka ambae ameamua kutoa maisha yake kunisaidia, sasa sijui nitampata wapi angalau nimpe shukurani zangu" Suzana usiku huo ilikuwa ni kuwaza tu kuhusu Novan lakini hakupata majibu ya maswali ila akiwa kwenye msongo wa mawazo simu yake ilianza kuita na aliekuwa anapiga alikuwa ni mama yake mkubwa. Hakutaka kumpuuzia alimpokelea na kumsikiliza alikuwa na mpya gani lakini alimsikia akiongea huku akiwa mwenye hofu sana ambayo ilimfanya Suzana ashindwe kufahamu nini kinaendelea. "Suzana mwanangu upo mzima kweli.!?" "Nipo mzima lakini mama mkubwa kwani shida nini mbona unaonekana ni mtu mwenye hofu sana nini kimekukuta.!?" "Oh asante Mungu uko mzima ila nilikukataza hayo mambo ya club na kutoka usiku ona sasa leo kidogo ufe yaani daah nimevurugwa.!!" "Mama kwani nani kakwambia mimi nilikuwa club pia nilitaka kufa mbona wanakudanganya, mimi sikwenda popote nilikuwa hapa hapa nyumbani nafuatulia mambo ya biashara zangu" "Sawa nifanye mtoto ila siku nyingine sihitaji kabisa utoke usiku na kama unataka kutoka basi uniage na iwe sehemu ya muhimu unaenda lakini kinyume na hapo basi sitakuelewa" "Sawa mama mkubwa nimekuelewa na nikutakie usiku mwema" Suzana ilibidi awe mpole na mdogo kama kidonge lakini alijua lazima taarifa hizo mama yake mkubwa amezipata kutoka kwa rafiki zake, huenda akawa Sabina au Sheila lakini alijua mmoja kati yao atakuwa amepeleka umbea kwa mama yake mkubwa. Ilibidi jambo hilo aliweke kiporo moyoni mwake, alivuta shuka na kuuchapa usingizi huku saa yake ya ukutani ikisoma ni saa nane kasoro usiku. ******************* Siku iliyofuata asubuhi na mapema ilikuwa siku ya Jumapili Novan aliamka mapema sana, licha ya maumivu aliyokuwa nayo mwilini lakini hakujali alifunga safari kuelekea kwenye duka la bidhaa za jumla na kununua bidhaa nyingi kisha alikodi gari na kuzipakia. Ilikuwa ni kawaida yake kila Jumapili kufanya hivyo na hua akinunua mahitaji hayo basi hupeleka katika kanisa kubwa ambalo pia hulea watoto yatima na hata yeye alikulia katika kanisa hilo. Basi alifikisha mahitaji hayo kanisani kisha alikutana na sister Maria ambae alikuwa ni sister mkubwa wa kanisa hilo na huyo ndie aliekuwa akimlea tangu alivyokuwa mdogo. "Novan lakini mbona kila Jumapili ukileta misaada unakuja mwenyewe simuoni mwenzako Nason au hataki kuja kuniona?" "Sijui sister na hata mimi hua namwambia sister Maria amekukumbuka sana anahitaji kukuona lakini anasema tu Jumapili ijayo naenda mara siku ikifika anasema yupo busy basi hata simuelewi" "Sawa kama yupo busy muache najua ipo siku atakuja" "Sawa sister Maria acha mimi niende maana nina harakati nyingi natakiwa nikazifanye basi Mungu akipenda tutaonana Jumapili ijayo na naweza kuja na Nason" Novan aliaga na kusindikizwa mpaka nnje ya kanisa. Kanisa hilo lilikuwa ni kubwa sana na lilikuwa karibu na barabara kuu hivyo wakati huo huo Suzana alikuwa akipita hapo hapo na gari yake ila alipotazama nnje ya kanisa alimuona Novan akizungumza na sister. Alishangaa sana kumuoma Novan hapo kanisani hivyo ilibidi aende mbele kidogo na kugeuza gari yake ili kurudi nyuma lakini akilini mwake bado alikuwa haelewi Novan anafanya nini kwenye kanisa halafu ukizingatia ni muuwaji. "Sasa yule muuwaji anafanya nini pale au ameenda kutubu dhambi zake za jana, hebu kwanza subiri nimfuate nikamuulize vizuri" Suzana alirudisha gari mpaka pale kanisani lakini alimkuta sister amesimama mwenyewe na Novan alikuwa tayari ameondoka. "Samahani sister nilikuwa namuulizia huyu kaka alietoka hapa sasa hivi ameelekea wapi?" "Kuwa mpole binti na karibu, naomba uingie kanisani tuzungumze kisha utafahamu ameelekea wapi usiwe na haraka hata Mungu hapendi" "Ok sawa sister" Suzana ilibidi awe mpole na kuingia kanisani, pia alikuwa akihitaji kujua Novan amefuata nini hapo mbona alimuona akiongea vizuri na sister ilhali alikuwa ni mtu mbaya sana. "Karibu sana binti sijafahamu unaitwa nani lakini najua una maswali mengi kuhusu Novan" "Novan..!?" "Novan ni nani lakini mimi naitwa Suzana Andew" "Jina zuri sana binti ila Novan ni kijana ambae umekuja hapa kumuulizia, yule ni kijana wangu ambae nimemlea tangu akiwa na miaka mitatu mpaka pale unapomuona sasa sifahamu kwanini unamuhitaji halafu unaonekana mwenye shauku sana.!" "Sister mimi nilikuwa namuhitaji yeye ili kumshukuru maana alinisaidia pia kumjua kiundani maisha yake na hapa alikuja kwa lengo gani.!" "Ah Novan ni kijana mpole sana na mwenye kutenda misaada kwa watu wenye uhitaji na hapa alikuja kuleta mahitaji kwaajili ya kuendelea kulea watoto pia anakuwa akifanya hivyo kila Jumapili na kwa miaka mingi sana" "Ahaaa kwahiyo Novan ndio yupo hivyo ila hakuna chochote unachojua zaidi kuhusu yeye.?" "Najua vingi hasa chakula anachopenda, wimbo na hata sehemu anazopenda kwenda kama kwenye sinema na vingine vingi" "Hapana sister namaanisha labda kazi anayofanya au maisha anayoishi?" "Anaishi vizuri tu pia anafanya kazi kwenye supermarket kiufupi hana mambo mengi sana" Sister alijibu kila anachokijua kumuhusu Novan lakini Suzana hakutaka kuongea neno jingine maana yeye anajua kama Novan ni muuwaji na jambo hilo hakutaka kumueleza sister, alimuaga na kiondoka zake. "Inamaana huyu kaka anaitwa Novan, sasa mbona jina zuri halafu ni mkatili sana pia moyo wake mzuri wa kutenda misaada halafu ni jambazi au anafosiwa kufanya haya?" Suzana akiwa kwenye gari alikuwa na maswali mengi sana ya kujiuliza kuhusu Novan pia hakufahamu atampata wapi ili ikiwezekana amjue kiundani zaidi hasa kazi anayofanya na maisha anayoishi. ******************* Majira taratibu yalianza kusogea mpaka inatimu saa sita mchana Suzana alikuwa tayari amefika nyumbaji kwa Sabina na safari yake ilikuwa ikimleta hapo, hakuwa yeye na Sabina tu pia alikuwa Sheila na wote kwa pamoja waliitwa hapo na Suzana. "Suzana mbona umeitisha huu mkusanyiko ghafla halafu unajua leo ni weekend ni siku ya kuenjoy na wapenzi zetu au unatuzuia kusudi ili tusiende kufurahi?" Alizungumza Sabina na kumfanya Suzana amtazame kwa muda kisha alipotezea. "Nyie kweli marafiki, yaani nilifikiri mtauliza nini kilitokea pale baada ya lile tukio ila ndio kwanza mnaanza kuongea shit ok sawa lakini sijapenda tabia yenu kumpigia simu mama mkubwa halafu kumwambia kilichotokea jana" "Lakini Suzana unafikiri tumefanya vibaya, sisi tumefanya ili kukusaidia wewe halafu unaanza kuja kutushutumu kweli wewe huna akili shoga yetu.!!" "Nyie ndio mmekosa akili badala ya kutafuta msaada nikomboke pale ndio kwanza mnakimbilia kusema umbea sijui mpoje ndio maana hamnenepi mnabaki kuwa kama sindano kwaajili ya umbea" Suzana alijikuta akipanic maana jambo walilofanya rafiki zake lilimkera sana. "Suzana naomba utoke kwangu naona sasa umeshindwa kukaa na kuongea vizuri, nenda bhana na najua akili zako zinatokana na kukosa mpenzi kwahiyo ondoka sitaki kukuona" "Ni sawa naondoka ila kesho mjiandae kuja kuchukua barua za kuacha kazi, siwezi kuwa na watu wapuuzi kwenye kampuni yangu" Suzana aliinuka na kuchukua mkoba wake lakini kiukweli alikuwa amechukia sana. "Usitutishe na hivyo vikampuni vyako vya pesa ya mawazo sawa, halafu kama ulikuwa hujui sisi ndio tulikuwa tunatia hasara kwenye kampuni yako, ulikuwa unaishi na virusi bila kujua sasa kaa ukijua" Kama kawaida ya majibizano ya wanawake maneno yalikuwa mengi na matusi ya kila aina lakini mwisho Suzana alitoka nnje, aliwasha gari yake na kuondoka zake huku akiwa mwingi wa hasira sana. Safari yake ilimfikisha supermarket kununua pombe lakini wakati anaingia alipigana kikumbo na mtu lakini yule mtu alimuomba samahani na kuondoka zake. Hakumfahamu alikuwa ni nani ila alipotezea, aliingia ndani na kuchagua pombe alizokuwa anazitaka lakini wakati anataka kulipa, anaingiza mkono kwenye mkoba hakuona chochote. "Mh inamaana sikuja na pesa au nimeziacha kwenye gari.!?" Suzana alihisi kuchanganyikiwa kidogo lakini wakati anakagua mkoba wake vizuri alifika mtu na kumlipia. "Asante sana kaka yangu" Alikuwa ni mwanaume fulani mtanashati ndiye alielipa pesa na mwanaume yule alionekana ni mtu mwenye pesa maana nguo alizovaa zilikuwa za gharama, pete za dhahabu na nyuma alikuwa na walinzi wawili waliokuwa wakimlinda. "Usijali dada mimi naitwa Noel sijui nani mwenzangu.?" "Ah naitwa Suzana" "Oh Suzana ni jina zuri na limekufaa kabisa maana wewe pia ni mzuri na unavutia sana" Mwanaume yule alianza kumtupia sifa kede kede Suzana ambae alijikuta akifurahi sana na kuenjoy lakini Suzana wakati anawatazama wale walinzi wa yule mwanaume alishangaa kumuona Novan na Nason ambao ndio waliokuwa wakimlinda na hii ikamfanya kichwa chake kijae maswali mengi sana.... ITAENDELEA..... SOMA MPAKA MWISHO KWA SH 1000 NJOO WHATSAPP 0743433005Story......... PENZI LA MTEKAJI 1......2 Mkasa...wa...kusisimua Sehemu Ya {01} Yapata kama majira ya saa sita mchana, hali ya hewa ilikuwa ya mawingu kuashiria mvua inataka kushuka, jua lilifichwa na mawingu mazito yaliyosindikizwa na upepo mwanana uliomfanya kila mmoja afurahie maana ulikuwa ukivuma taratibu sana. Wakati hali hiyo inaendelea katika ofisi moja ya kampuni ambayo inajishughulisha na maswala ya fashion walionekana mabinti watatu wameketi wakizungumza na mabinti hao walikuwa ni watu wa karibu sana. Walikuwa wakiongea mengi sana lakini kubwa zaidi waligusia swala la mahusiano na kila mmoja alikuwa akisifia mahusiano yake lakini binti mmoja alikuwa kimya na ndie aliekuwa bosi wa kampuni hiyo. Huenda ikawa hana mpenzi au mapenzi yake yalikuwa na mgogoro hilo halikujulikana lakini alionekana kuwa kimya akiwatazama wenzake. "Lakini Suzana we nawe umezidi bosi yaani kila mwanaume anaekutokea na kukutongoza unamkataa sasa sijui unahitaji mwanaume wa aina gani jamani.!!" Alizungumza mwanamke mmoja mweupe mnene ambae nae alikuwa ni miongoni mwa wanawake hao. "Hebu Sabina muache bhana huenda anataka kuja kuolewa na Rais" "Sasa Raisi gani tena wakati Raisi wetu mama Samia ni wa kike au anataka kuja kuolewa na Hussein Mwinyi Raisi wa Zanzibar.!!" Basi yalikuwa ni maongezi yaliyojaa utani lakini Suzana alikuwa kimya akiwasikiliza na pia hakuwa muongeaji sana alibaki kuwatazama wenzake waliozidi kumsema.. "Jamani kama mmemaliza kunisema haya tokeni muende kuendelea na majukumu yenu maana mnaona humu kama sehemu ya kuongea umbea haya inukeni na mtoke" Suzana alikuwa amechukia kiasi chake na hakutaka kuendelea kusikiliza maongezi yao hivyo aliona awafukuze ili kuondoa kero. Basi wale mabinti yaani Sabina na mwenzake Sheila ilibidi wainuke na kuondoka zao wakimuacha Suzana kwenye mawazo mengi, haelewi aanze wapi aishie wapi. "Lakini wanachosema wenzangu ni kweli naweza kuzeeka bila kupata mpenzi sasa acha nitafute mh hapana siwezi kutafuta nikaonekana mwanamke rahisi najua nitafuatwa tu" Suzana baada ya kubaki mwenyewe aliyawaza hayo na mwisho alichukua peni pamoja na karatasi kisha alitoka nje kwenda kuangalia maendeleo ya vijana wake aliowaajiri kama wanafanya kazi kwa ufasaha. Suzana alikuwa ni binti wa miaka 23 binti aliekuwa na pesa nyingi sana ambazo amezirithi kutoka kwa wazazi wake, pia Suzana alikuwa akiishi na mama yake mkubwa ambae ndie amemlea tangu wazazi kufariki mpaka anakuwa na kujielewa. Kingine Suzana alikuwa ni binti mkimya asiependa mazoea ovyo na hiyo ndio ilipelekea mpaka wakati huo kuishi bila mpenzi na mama yake mkubwa alikuwa akimsisitiza kila siku kutafuta mwenza lakini alipotezea. Basi tutoke huko sasa kwa Suzana tuje upande wa pili ambapo huku alionekana kuna kijana wa makamo akiwa chumbani kwake katika nyumba ya kupanga na kulikuwa ni uswahilini hivyo kelele za watoto zilisikika nnje ya chumba chake. Kelele hizo za watoto hazikumfanya kushindwa kufanya kazi yake na wakati huo alikuwa busy kusafisha bastola yake ambayo hiyo huitumia muda mwingi katika majukumu yake. Kijana huyo alifahamika kwa jina la Novan na alikuwa kijana mpole, aliependa jamii inayo mzunguka lakini licha ya upole wake ila alikuwa ni kijana anaetumiwa kihalifu hasa katika mambo ya utakaji na uuwaji. Wakati yupo busy kusafisha bastola yake mara simu yake ilianza kuita hivyo aliichukua na kupokea kisha aliweka sikioni. "Hey Novan unahitajika na bosi usiku wa leo kwahiyo ifikapo majira ya saa mbili uwe hapa kuna jukumu linawahusu hapa" "Ok sawa haina shida" Baada ya simu hiyo kukatwa aliweka simu yake kando na kuendelea na zoezi lake la kusafisha bastola, hakuwa na papara wala wasiwasi. Novan alikuwa ni kijana wa miaka 24, kijana mpole na asiependa kuongea sana lakini upole wake ulificha uhalisia wake machoni mwa watu, alikuwa ni kijana mbaya sana ambae kuuwa kwake ilikuwa kama starehe. ***************** Muda ulikwenda, ilipotimu majira ya saa moja usiku Novan alijiandaa vyema kwa kuvalia mavazi yake meusi, alipachika bastola yake kiunoni na kutoa pikipiki yake kubwa ya kisasa ambayo muda mwingi huitumia katika safari zake. Alijipakia na kuanza safari kuelekea makao makuu yao lakini hakujua ni kazi gani ambayo wanakwenda kufanya siku hiyo, either ya utekaji au ya mauaji. Kutokana na kasi ya pikipiki yake alitumia takribani dakika thelathini kufika katika supermarket moja ambayo alipaki pikipiki yake nnje na kushuka, alitazama kushoto na kulia kisha aliingia kwenye supermarket hiyo. Ilikuwa ni supermarket kubwa ambayo hujihusisha na uuzaji wa bidhaa mbali mbali lakini ndani ya supermarket hiyo kulikuwa na mlango wa siri ambao Novan aliingia na kutokea chini ya supermarket ambapo huko ndipo shughuli na mipango yao hufanyika. Alifika na kupokelewa vizuri maana walikuwa wakiijua kazi yake, akipewa jukumu alitimize basi kufeli kwake ni mara chache sana lakini mara nyingi lazima afanya kazi kwa ufasaha na kuikamilisha. "Nafurahi umefika kwa wakati Novan, sasa leo hatuna mission ya utekaji wa mabinti ila leo mtakwenda kwenye club ya santiago ambapo Mr Moses leo anakutaka na tajiri kutoka uturuki kwahiyo nahitaji mumuangamize" Alizungumza bosi au mkuu ambae ndie anawapa mission za kufanya. "Lakini mkuu unajua jinsi gani Mr Moses alivyo na ulinzi sasa huoni kama itakuwa ni ngumu kwetu halafu umetuchagua sisi wawili tu.!?" "Usijali Nason nimewachagua kwasababu nawaamini kwahiyo kwa kushirikiana wewe na Novan naamini mtamaliza jukumu hili na leo nitawapa pesa nzuri endapo mtamuuwa Mr Moses" "Ok sawa" Ilibidi Nason na Novan watoke hapo na kuanza safari kuelekea santiago club ambapo huko ndipo walipangiwa mission. Walitumia usafiri wa gari yao binafsi lakini wakiwa ndani ya gari story pia zilichukua nafasi yake. "Hivi Novan unajua hii kazi nafanya basi tu lakini natamani leo kesho niache maana tunafanya kazi ngumu lakini malipo kidogo, haturuhusiwi kuwa na wapenzi sasa si kama jela tu.!?" "Yah lakini si unajua sheria, kama utajihusisha kimapenzi na mwanamke halafu ukagundulika kinachofuata ni kifo wewe na mtu wako, kwahiyo kaa kwa kutulia mtu wangu tufanye majuku yetu" Novan ilibidi amkumbushe tu Nason huku safari ikichana mawimbi ya barabara kuitafuta santiago club ambayo ilikuwa nnje kidogo ya mji. Wakati safari yao inaendelea huku kwa Suzana alifuatwa na rafiki zake usiku huo na walikuwa wamevalia vizuri kuashiria kuna sehemu walikuwa wanaenda. "Sasa jamani ndio kunifuata usiku nyumbani nataka kulala halafu mbona mmependeza kiasi hicho kulikoni tena.!?" Suzana alibaki kuwatazama wenzake na kuwauliza maana ilionesha walikuwa na safari. "We nae jamani mara hii umesahau wakati tulipanga kwenda santiago club halafu nimepata taarifa kuna band nyingi zitakuwepo, shisha za kumwaga kwahiyo tusichelewe dada fanya haraka twende" "Aaah halafu nilikuwa nimesahau kabisa ok basi sawa nisubiri nijiandae halafu tuelekee huko maana bado muda unaruhusu" Suzana haraka alirudi ndani na bahati nzuri mama yake mkubwa alikuwa amesafiri muda mrefu sana hivyo ikawa kwake huru kufanya chochote. Takribani dakika kumi na tano alizitumia kujiandaa, alipomaliza haraka alitoka na safari ilianza kuelekea santiago club ambapo huko huko Nason na Novan walikuwa wanaenda kufanya jukumu lao la kumuuwa Mr Moses. ******************* Club ilikuwa imefurika, watu kutoka sehemu mbali mbali ya jiji walifika hapo na katika umati huo ndani yake walikuwa marafiki watatu yaani Suzana, Sabina na Sheila, walikuwa wakiangaza huku na kule kutafuta meza nzuri ambayo wangeketi na kupata vinywaji. "Jamani hebu twendeni kuketi kwenye meza ile" Baada ya kuona meza wote kwa pamoja walisogea na kuketi lakini sehemu waliyokaa wao ilikuwa karibu kabisa na sehemu ambayo maongezi ya Mr Moses na tajiri kutoka uturuki yalikuwa yanaendelea na jambo kubwa walikuwa wakiongea kuhusu biashara. Walikuwa hawana ili wala lile na muda huo huo Nason na Novan walifika kama wateja, walitafuta meza na kuketi kisha waliagiza vinywaji ambavyo hawakuvitumia ila waliweka kama urembo huku wakimsomea ramani Mr Moses. Masikioni mwao walikuwa na vibluetooth vidogo ambavyo waliweza kuongea na mkuu wao akiwapa maelekezo nini cha kufanya. "Mkuu tayari tumemuona Mr Moses ila hana ulinzi mkubwa ana vijana wawili tu waliomsimamia pembeni" "Basi muuweni mara moja ila huyo mturuki mumuache maana bosi anamuhitaji kufanya nae biashara, hapo cha kufanya ua huyo Mr Moses ambae ndie kikwazo cha biashara" "Ok sawa" Baada ya mawasiliano hayo Novan na Nason hawakuchelewa walificha nyuso zao kwa mask kisha walipeana signal na kuanza kuwashambulia wale walinzi ili kupata nafasi ya kumuuwa Mr Moses. Risasi mbili zilisikika zilizowaangusha wale walinzi wa Mr Moses chini lakini milio ya risasi hiyo iliwafanya watu kutaharuki na kuanza kukimbia ovyo kutafuta njia ya kutokea humo. Upande wa Mr Moses alijua tayari amekuja kuuwawa maana muda mwingi alikuwa akiwindwa hivyo aliona njia ya kutoka hapo salama ni kumchukua mtu kama ngao ili aweze kukimbia. Alimsogelea kijana wake mmoja aliekuwa chini kisha alichukua bastola na kumvamia binti mmoja aliepita mbele yake ili kumfanya kama ngao na bahati mbaya alikuwa amempata alikua ni Suzana ambae alijikuta akipiga kelele kuomba aachiwe. "We binti tulia mimi siwezi kukuuwa ila nitakufanya kama ngao sasa kama ukileta ubishi nitabomoa kichwa chako" Suzana ilibidi awe mpole kuhofia kufa lakini Nason na Novan walipoona Mr Moses amemtumia mtu kama ngao ilibidi wasogee kwa kujiamini maana walijua hatoweza kufanya chochote. "We mzee hebu acha ujinga sasa unafikiri tukiamua kukuuwa tunashindwa, yaani tunakuuwa wewe na huyo mwanamke kwahiyo muachie huyo binti aende sisi tunataka tudeal na wewe tu" Novan alizungumza huku akisogea zaidi na kumfanya Mr Moses aanze kutetemeka kwa hofu huku kwa Suzana alihisi haja kubwa kumtoka maana mdomo wa bastola ulikuwa kichwani kwake. "Na...nase...nasema asisogee mtu nitaua naombeni mkae mbali, kwanza vueni hizo mask niwaone sura zenu ni wakina nani nyie...!! "Haina haja ya kuvua wewe tunaomba muachie huyo binti aende halafu tutakuacha salama ila kinyume na hapo utakufa" "Sasa nitamshoot risasi kama hamtafanya ninachowaambia" "Ok sawa kuwa mtulivu tutatoa hizi mask lakini umuachie huyo binti" Novan licha ya kuwa muuwaji na mtekaji lakini hakupenda kuona watu wasio na hatia wakifa hivyo ilibidi akubali kuvua mask na kupelekea sura yake kuonekana. "Sasa Novan umefanya nini.!?" "Tulia Nason huyu mzee mbona tutamuuwa wala usijali kwahiyo hapa namzuga tu halafu wewe kaa tayari kumshoot" Mr Moses hakujua kama mipango ilikuwa inapangwa kwa siri, baada ya kuona sura ya Novan alimsukuma Suzana kuelekea alipo Novan kisha alifyatua risasi mbili zilizokuwa zikienda kumpiga Suzana mgongoni lakini Novan aliwahi, alimgeuza Suzana na zile risasi mbili zilipiga mgongoni kwake huku Nason alipata nafasi ya kumshambulia Mr Moses na kumuua.... ITAENDELEA... Story......... PENZI LA MTEKAJI Mkasa...wa...kusisimua Sehemu Ya {02} ILIPOISHIA...... Mr Moses hakujua kama mipango ilikuwa inapangwa kwa siri, baada ya kuona sura ya Novan alimsukuma Suzana kuelekea alipo Novan kisha alifyatua risasi mbili zilizokuwa zikienda kumpiga Suzana mgongoni lakini Novan aliwahi, alimgeuza Suzana na zile risasi mbili zilipiga mgongoni kwake huku Nason alipata nafasi ya kumshambulia Mr Moses na kumuua. ENDELEA NAYO..... Novan alikuwa chini akigugumia kwa maumivu huku damu nyingi sana zikimtoka mgongoni kwake pia upande wa Suzana alikuwa bado mwenye hofu maana alikuwa amenusurika kwenye tundu la sindano pia asingekuwa Novan kukinga risasi basi muda huo angekuwa yeye ndiye anaugulia maumivu ya risasi. "Ka...kaka yangu unaendelaje.!!?" Suzana alisogea mpaka alipo Novan na kumuuliza lakini hakujibiwa kitu, Novan alichukua mask yake na kuirudisha usoni. Wakati huo huo Nason alimchukua na kuondoka nae hawakutaka kabisa kuongea chochote na Suzana walimuacha akiwa mwenye maswali mengi na kujiuliza wale walikuwa ni watu wa aina gani lakini hakupata jibu la kuridhisha akili yake. Wakati Novan na Nason wanaondoka huku nyuma jeshi la polisi likifika baada ya kupata taarifa za uvamizi kwenye club ila walifika na kukuta mashambulizi yamefanyika na kilichobaki ni damu na maiti ya Mr Moses tu. Walitazama pembeni walimuona Suzana ameketi huku akitetemeka kwa hofu, ilibidi wamfuate na kuanza kumuhoji inawezekana wakapata chochote kutoka kwake na wakawajua wahalifu kwa ufupi. "Samahani dada kwanza pole sana kwa kilichotokea hapa najua akili yako haiko sawa kwa sasa lakini nahitaji kujua mawili matatu kwa kilichotokea hapa.?" Askari mmoja wa kike alimfuata Suzana na kuanza kumuuliza maswali lakini Suzana alikuwa mzito kujibu na hata mdomo wake kuufungua aliona kama umefungwa vyuma. "Dada hebu jitahidi japo utueleze machache kuhusu tukio lililotokea hapa lakini ukikaa kimya tutashindwa kufahamu tuanzie wapi tuishie wapi" "Mi...mimi sijui chochote lakini watu waliovaa mask usoni mwao ndio wamefanya hivi lakini kingine sifahamu" "Ok sawa aina shida cctv camera zipo tutaangalia kwahiyo tunaomba uende nyumbani ukapumzike ili akili ikae sawa acha sisi tufanye kazi yetu" Askari ilibidi wamruhusu Suzana kuondoka lakini hata tembea yake ilikuwa kama mtoto mdogo anaejifunza kutembea, basi alitoka mpaka nnje na bahati nzuri kwenye club hiyo kulikuwa na tax nyingi za usafiri zimepaki nnje hivyo aliingia kwenye tax moja wapo na kuomba apelekwe kwake. Wakati hayo yanaendelea Nason alimfikisha Novan kwake na kuanza kumfanyia huduma ya kwanza, alikuwa akimtoa risasi mgongoni pasi na ganzi kisha alimfunga vizuri bandage na kuanza kupiga story zao. "Yaani Novan sasa ulifanya nini pale kumtetea yule binti, mimi nilijua labda utampiga risasi pamoja na Mr Moses na baada yake wewe ndiye umepigwa risasi.!" "Ah sikutaka yule binti afe halafu sisi hatuui watu ovyo ila tunauwa waliokuwa katika target yetu kwahiyo nikaona nimsaidie ila kikubwa mission passed tunatakiwa tukapeleke majibu makao makuu" "Ok sawa haina shida" Novan na Nason walichukuzana hapo na kuelekea makao makuu yao ambapo huko walipokelewa vizuri na taarifa zile zilimfurahisha sana bosi. "Vijana mmefanya kazi kwa weledi mkubwa sana japo kuna makosa mmefanya lakini siku nyingine mabinti kama wale mnaua hakuna kutetea maana unaweza ukajikuta unakufa wewe" "Ok sawa mkuu" Siku hiyo ilifanyika part kwa wahalifu hao lakini Novan hakuweza kuhudhuria maana alikuwa na maumivu makali sana mgongoni hivyo aliomba ruhusu na kurudi kwake kupumzika. Wakati yeye amepumzika kwake na huku Suzana alikuwa amefika kwake muda sana lakini alifikia kupanda kitandani bila kuoga na kuutafuta usingizi ambao ulipeperushwa na mawazo ya tukio lilotokea masaa machache nyuma. "Lakini yule kaka kwanini amenisaidia mimi wakati mimi najua wahalifu hawajali hata mtu akifa kikubwa watimize jukumu lao.!?" "Ila sifikirii kama wahalifu wote watakuwa na roho mbaya, wapo wazuri kama yule kaka ambae ameamua kutoa maisha yake kunisaidia, sasa sijui nitampata wapi angalau nimpe shukurani zangu" Suzana usiku huo ilikuwa ni kuwaza tu kuhusu Novan lakini hakupata majibu ya maswali ila akiwa kwenye msongo wa mawazo simu yake ilianza kuita na aliekuwa anapiga alikuwa ni mama yake mkubwa. Hakutaka kumpuuzia alimpokelea na kumsikiliza alikuwa na mpya gani lakini alimsikia akiongea huku akiwa mwenye hofu sana ambayo ilimfanya Suzana ashindwe kufahamu nini kinaendelea. "Suzana mwanangu upo mzima kweli.!?" "Nipo mzima lakini mama mkubwa kwani shida nini mbona unaonekana ni mtu mwenye hofu sana nini kimekukuta.!?" "Oh asante Mungu uko mzima ila nilikukataza hayo mambo ya club na kutoka usiku ona sasa leo kidogo ufe yaani daah nimevurugwa.!!" "Mama kwani nani kakwambia mimi nilikuwa club pia nilitaka kufa mbona wanakudanganya, mimi sikwenda popote nilikuwa hapa hapa nyumbani nafuatulia mambo ya biashara zangu" "Sawa nifanye mtoto ila siku nyingine sihitaji kabisa utoke usiku na kama unataka kutoka basi uniage na iwe sehemu ya muhimu unaenda lakini kinyume na hapo basi sitakuelewa" "Sawa mama mkubwa nimekuelewa na nikutakie usiku mwema" Suzana ilibidi awe mpole na mdogo kama kidonge lakini alijua lazima taarifa hizo mama yake mkubwa amezipata kutoka kwa rafiki zake, huenda akawa Sabina au Sheila lakini alijua mmoja kati yao atakuwa amepeleka umbea kwa mama yake mkubwa. Ilibidi jambo hilo aliweke kiporo moyoni mwake, alivuta shuka na kuuchapa usingizi huku saa yake ya ukutani ikisoma ni saa nane kasoro usiku. ******************* Siku iliyofuata asubuhi na mapema ilikuwa siku ya Jumapili Novan aliamka mapema sana, licha ya maumivu aliyokuwa nayo mwilini lakini hakujali alifunga safari kuelekea kwenye duka la bidhaa za jumla na kununua bidhaa nyingi kisha alikodi gari na kuzipakia. Ilikuwa ni kawaida yake kila Jumapili kufanya hivyo na hua akinunua mahitaji hayo basi hupeleka katika kanisa kubwa ambalo pia hulea watoto yatima na hata yeye alikulia katika kanisa hilo. Basi alifikisha mahitaji hayo kanisani kisha alikutana na sister Maria ambae alikuwa ni sister mkubwa wa kanisa hilo na huyo ndie aliekuwa akimlea tangu alivyokuwa mdogo. "Novan lakini mbona kila Jumapili ukileta misaada unakuja mwenyewe simuoni mwenzako Nason au hataki kuja kuniona?" "Sijui sister na hata mimi hua namwambia sister Maria amekukumbuka sana anahitaji kukuona lakini anasema tu Jumapili ijayo naenda mara siku ikifika anasema yupo busy basi hata simuelewi" "Sawa kama yupo busy muache najua ipo siku atakuja" "Sawa sister Maria acha mimi niende maana nina harakati nyingi natakiwa nikazifanye basi Mungu akipenda tutaonana Jumapili ijayo na naweza kuja na Nason" Novan aliaga na kusindikizwa mpaka nnje ya kanisa. Kanisa hilo lilikuwa ni kubwa sana na lilikuwa karibu na barabara kuu hivyo wakati huo huo Suzana alikuwa akipita hapo hapo na gari yake ila alipotazama nnje ya kanisa alimuona Novan akizungumza na sister. Alishangaa sana kumuoma Novan hapo kanisani hivyo ilibidi aende mbele kidogo na kugeuza gari yake ili kurudi nyuma lakini akilini mwake bado alikuwa haelewi Novan anafanya nini kwenye kanisa halafu ukizingatia ni muuwaji. "Sasa yule muuwaji anafanya nini pale au ameenda kutubu dhambi zake za jana, hebu kwanza subiri nimfuate nikamuulize vizuri" Suzana alirudisha gari mpaka pale kanisani lakini alimkuta sister amesimama mwenyewe na Novan alikuwa tayari ameondoka. "Samahani sister nilikuwa namuulizia huyu kaka alietoka hapa sasa hivi ameelekea wapi?" "Kuwa mpole binti na karibu, naomba uingie kanisani tuzungumze kisha utafahamu ameelekea wapi usiwe na haraka hata Mungu hapendi" "Ok sawa sister" Suzana ilibidi awe mpole na kuingia kanisani, pia alikuwa akihitaji kujua Novan amefuata nini hapo mbona alimuona akiongea vizuri na sister ilhali alikuwa ni mtu mbaya sana. "Karibu sana binti sijafahamu unaitwa nani lakini najua una maswali mengi kuhusu Novan" "Novan..!?" "Novan ni nani lakini mimi naitwa Suzana Andew" "Jina zuri sana binti ila Novan ni kijana ambae umekuja hapa kumuulizia, yule ni kijana wangu ambae nimemlea tangu akiwa na miaka mitatu mpaka pale unapomuona sasa sifahamu kwanini unamuhitaji halafu unaonekana mwenye shauku sana.!" "Sister mimi nilikuwa namuhitaji yeye ili kumshukuru maana alinisaidia pia kumjua kiundani maisha yake na hapa alikuja kwa lengo gani.!" "Ah Novan ni kijana mpole sana na mwenye kutenda misaada kwa watu wenye uhitaji na hapa alikuja kuleta mahitaji kwaajili ya kuendelea kulea watoto pia anakuwa akifanya hivyo kila Jumapili na kwa miaka mingi sana" "Ahaaa kwahiyo Novan ndio yupo hivyo ila hakuna chochote unachojua zaidi kuhusu yeye.?" "Najua vingi hasa chakula anachopenda, wimbo na hata sehemu anazopenda kwenda kama kwenye sinema na vingine vingi" "Hapana sister namaanisha labda kazi anayofanya au maisha anayoishi?" "Anaishi vizuri tu pia anafanya kazi kwenye supermarket kiufupi hana mambo mengi sana" Sister alijibu kila anachokijua kumuhusu Novan lakini Suzana hakutaka kuongea neno jingine maana yeye anajua kama Novan ni muuwaji na jambo hilo hakutaka kumueleza sister, alimuaga na kiondoka zake. "Inamaana huyu kaka anaitwa Novan, sasa mbona jina zuri halafu ni mkatili sana pia moyo wake mzuri wa kutenda misaada halafu ni jambazi au anafosiwa kufanya haya?" Suzana akiwa kwenye gari alikuwa na maswali mengi sana ya kujiuliza kuhusu Novan pia hakufahamu atampata wapi ili ikiwezekana amjue kiundani zaidi hasa kazi anayofanya na maisha anayoishi. ******************* Majira taratibu yalianza kusogea mpaka inatimu saa sita mchana Suzana alikuwa tayari amefika nyumbaji kwa Sabina na safari yake ilikuwa ikimleta hapo, hakuwa yeye na Sabina tu pia alikuwa Sheila na wote kwa pamoja waliitwa hapo na Suzana. "Suzana mbona umeitisha huu mkusanyiko ghafla halafu unajua leo ni weekend ni siku ya kuenjoy na wapenzi zetu au unatuzuia kusudi ili tusiende kufurahi?" Alizungumza Sabina na kumfanya Suzana amtazame kwa muda kisha alipotezea. "Nyie kweli marafiki, yaani nilifikiri mtauliza nini kilitokea pale baada ya lile tukio ila ndio kwanza mnaanza kuongea shit ok sawa lakini sijapenda tabia yenu kumpigia simu mama mkubwa halafu kumwambia kilichotokea jana" "Lakini Suzana unafikiri tumefanya vibaya, sisi tumefanya ili kukusaidia wewe halafu unaanza kuja kutushutumu kweli wewe huna akili shoga yetu.!!" "Nyie ndio mmekosa akili badala ya kutafuta msaada nikomboke pale ndio kwanza mnakimbilia kusema umbea sijui mpoje ndio maana hamnenepi mnabaki kuwa kama sindano kwaajili ya umbea" Suzana alijikuta akipanic maana jambo walilofanya rafiki zake lilimkera sana. "Suzana naomba utoke kwangu naona sasa umeshindwa kukaa na kuongea vizuri, nenda bhana na najua akili zako zinatokana na kukosa mpenzi kwahiyo ondoka sitaki kukuona" "Ni sawa naondoka ila kesho mjiandae kuja kuchukua barua za kuacha kazi, siwezi kuwa na watu wapuuzi kwenye kampuni yangu" Suzana aliinuka na kuchukua mkoba wake lakini kiukweli alikuwa amechukia sana. "Usitutishe na hivyo vikampuni vyako vya pesa ya mawazo sawa, halafu kama ulikuwa hujui sisi ndio tulikuwa tunatia hasara kwenye kampuni yako, ulikuwa unaishi na virusi bila kujua sasa kaa ukijua" Kama kawaida ya majibizano ya wanawake maneno yalikuwa mengi na matusi ya kila aina lakini mwisho Suzana alitoka nnje, aliwasha gari yake na kuondoka zake huku akiwa mwingi wa hasira sana. Safari yake ilimfikisha supermarket kununua pombe lakini wakati anaingia alipigana kikumbo na mtu lakini yule mtu alimuomba samahani na kuondoka zake. Hakumfahamu alikuwa ni nani ila alipotezea, aliingia ndani na kuchagua pombe alizokuwa anazitaka lakini wakati anataka kulipa, anaingiza mkono kwenye mkoba hakuona chochote. "Mh inamaana sikuja na pesa au nimeziacha kwenye gari.!?" Suzana alihisi kuchanganyikiwa kidogo lakini wakati anakagua mkoba wake vizuri alifika mtu na kumlipia. "Asante sana kaka yangu" Alikuwa ni mwanaume fulani mtanashati ndiye alielipa pesa na mwanaume yule alionekana ni mtu mwenye pesa maana nguo alizovaa zilikuwa za gharama, pete za dhahabu na nyuma alikuwa na walinzi wawili waliokuwa wakimlinda. "Usijali dada mimi naitwa Noel sijui nani mwenzangu.?" "Ah naitwa Suzana" "Oh Suzana ni jina zuri na limekufaa kabisa maana wewe pia ni mzuri na unavutia sana" Mwanaume yule alianza kumtupia sifa kede kede Suzana ambae alijikuta akifurahi sana na kuenjoy lakini Suzana wakati anawatazama wale walinzi wa yule mwanaume alishangaa kumuona Novan na Nason ambao ndio waliokuwa wakimlinda na hii ikamfanya kichwa chake kijae maswali mengi sana.... ITAENDELEA..... SOMA MPAKA MWISHO KWA SH 1000 NJOO WHATSAPP 0743433005Story......... PENZI LA MTEKAJI 1......2 Mkasa...wa...kusisimua Sehemu Ya {01} Yapata kama majira ya saa sita mchana, hali ya hewa ilikuwa ya mawingu kuashiria mvua inataka kushuka, jua lilifichwa na mawingu mazito yaliyosindikizwa na upepo mwanana uliomfanya kila mmoja afurahie maana ulikuwa ukivuma taratibu sana. Wakati hali hiyo inaendelea katika ofisi moja ya kampuni ambayo inajishughulisha na maswala ya fashion walionekana mabinti watatu wameketi wakizungumza na mabinti hao walikuwa ni watu wa karibu sana. Walikuwa wakiongea mengi sana lakini kubwa zaidi waligusia swala la mahusiano na kila mmoja alikuwa akisifia mahusiano yake lakini binti mmoja alikuwa kimya na ndie aliekuwa bosi wa kampuni hiyo. Huenda ikawa hana mpenzi au mapenzi yake yalikuwa na mgogoro hilo halikujulikana lakini alionekana kuwa kimya akiwatazama wenzake. "Lakini Suzana we nawe umezidi bosi yaani kila mwanaume anaekutokea na kukutongoza unamkataa sasa sijui unahitaji mwanaume wa aina gani jamani.!!" Alizungumza mwanamke mmoja mweupe mnene ambae nae alikuwa ni miongoni mwa wanawake hao. "Hebu Sabina muache bhana huenda anataka kuja kuolewa na Rais" "Sasa Raisi gani tena wakati Raisi wetu mama Samia ni wa kike au anataka kuja kuolewa na Hussein Mwinyi Raisi wa Zanzibar.!!" Basi yalikuwa ni maongezi yaliyojaa utani lakini Suzana alikuwa kimya akiwasikiliza na pia hakuwa muongeaji sana alibaki kuwatazama wenzake waliozidi kumsema.. "Jamani kama mmemaliza kunisema haya tokeni muende kuendelea na majukumu yenu maana mnaona humu kama sehemu ya kuongea umbea haya inukeni na mtoke" Suzana alikuwa amechukia kiasi chake na hakutaka kuendelea kusikiliza maongezi yao hivyo aliona awafukuze ili kuondoa kero. Basi wale mabinti yaani Sabina na mwenzake Sheila ilibidi wainuke na kuondoka zao wakimuacha Suzana kwenye mawazo mengi, haelewi aanze wapi aishie wapi. "Lakini wanachosema wenzangu ni kweli naweza kuzeeka bila kupata mpenzi sasa acha nitafute mh hapana siwezi kutafuta nikaonekana mwanamke rahisi najua nitafuatwa tu" Suzana baada ya kubaki mwenyewe aliyawaza hayo na mwisho alichukua peni pamoja na karatasi kisha alitoka nje kwenda kuangalia maendeleo ya vijana wake aliowaajiri kama wanafanya kazi kwa ufasaha. Suzana alikuwa ni binti wa miaka 23 binti aliekuwa na pesa nyingi sana ambazo amezirithi kutoka kwa wazazi wake, pia Suzana alikuwa akiishi na mama yake mkubwa ambae ndie amemlea tangu wazazi kufariki mpaka anakuwa na kujielewa. Kingine Suzana alikuwa ni binti mkimya asiependa mazoea ovyo na hiyo ndio ilipelekea mpaka wakati huo kuishi bila mpenzi na mama yake mkubwa alikuwa akimsisitiza kila siku kutafuta mwenza lakini alipotezea. Basi tutoke huko sasa kwa Suzana tuje upande wa pili ambapo huku alionekana kuna kijana wa makamo akiwa chumbani kwake katika nyumba ya kupanga na kulikuwa ni uswahilini hivyo kelele za watoto zilisikika nnje ya chumba chake. Kelele hizo za watoto hazikumfanya kushindwa kufanya kazi yake na wakati huo alikuwa busy kusafisha bastola yake ambayo hiyo huitumia muda mwingi katika majukumu yake. Kijana huyo alifahamika kwa jina la Novan na alikuwa kijana mpole, aliependa jamii inayo mzunguka lakini licha ya upole wake ila alikuwa ni kijana anaetumiwa kihalifu hasa katika mambo ya utakaji na uuwaji. Wakati yupo busy kusafisha bastola yake mara simu yake ilianza kuita hivyo aliichukua na kupokea kisha aliweka sikioni. "Hey Novan unahitajika na bosi usiku wa leo kwahiyo ifikapo majira ya saa mbili uwe hapa kuna jukumu linawahusu hapa" "Ok sawa haina shida" Baada ya simu hiyo kukatwa aliweka simu yake kando na kuendelea na zoezi lake la kusafisha bastola, hakuwa na papara wala wasiwasi. Novan alikuwa ni kijana wa miaka 24, kijana mpole na asiependa kuongea sana lakini upole wake ulificha uhalisia wake machoni mwa watu, alikuwa ni kijana mbaya sana ambae kuuwa kwake ilikuwa kama starehe. ***************** Muda ulikwenda, ilipotimu majira ya saa moja usiku Novan alijiandaa vyema kwa kuvalia mavazi yake meusi, alipachika bastola yake kiunoni na kutoa pikipiki yake kubwa ya kisasa ambayo muda mwingi huitumia katika safari zake. Alijipakia na kuanza safari kuelekea makao makuu yao lakini hakujua ni kazi gani ambayo wanakwenda kufanya siku hiyo, either ya utekaji au ya mauaji. Kutokana na kasi ya pikipiki yake alitumia takribani dakika thelathini kufika katika supermarket moja ambayo alipaki pikipiki yake nnje na kushuka, alitazama kushoto na kulia kisha aliingia kwenye supermarket hiyo. Ilikuwa ni supermarket kubwa ambayo hujihusisha na uuzaji wa bidhaa mbali mbali lakini ndani ya supermarket hiyo kulikuwa na mlango wa siri ambao Novan aliingia na kutokea chini ya supermarket ambapo huko ndipo shughuli na mipango yao hufanyika. Alifika na kupokelewa vizuri maana walikuwa wakiijua kazi yake, akipewa jukumu alitimize basi kufeli kwake ni mara chache sana lakini mara nyingi lazima afanya kazi kwa ufasaha na kuikamilisha. "Nafurahi umefika kwa wakati Novan, sasa leo hatuna mission ya utekaji wa mabinti ila leo mtakwenda kwenye club ya santiago ambapo Mr Moses leo anakutaka na tajiri kutoka uturuki kwahiyo nahitaji mumuangamize" Alizungumza bosi au mkuu ambae ndie anawapa mission za kufanya. "Lakini mkuu unajua jinsi gani Mr Moses alivyo na ulinzi sasa huoni kama itakuwa ni ngumu kwetu halafu umetuchagua sisi wawili tu.!?" "Usijali Nason nimewachagua kwasababu nawaamini kwahiyo kwa kushirikiana wewe na Novan naamini mtamaliza jukumu hili na leo nitawapa pesa nzuri endapo mtamuuwa Mr Moses" "Ok sawa" Ilibidi Nason na Novan watoke hapo na kuanza safari kuelekea santiago club ambapo huko ndipo walipangiwa mission. Walitumia usafiri wa gari yao binafsi lakini wakiwa ndani ya gari story pia zilichukua nafasi yake. "Hivi Novan unajua hii kazi nafanya basi tu lakini natamani leo kesho niache maana tunafanya kazi ngumu lakini malipo kidogo, haturuhusiwi kuwa na wapenzi sasa si kama jela tu.!?" "Yah lakini si unajua sheria, kama utajihusisha kimapenzi na mwanamke halafu ukagundulika kinachofuata ni kifo wewe na mtu wako, kwahiyo kaa kwa kutulia mtu wangu tufanye majuku yetu" Novan ilibidi amkumbushe tu Nason huku safari ikichana mawimbi ya barabara kuitafuta santiago club ambayo ilikuwa nnje kidogo ya mji. Wakati safari yao inaendelea huku kwa Suzana alifuatwa na rafiki zake usiku huo na walikuwa wamevalia vizuri kuashiria kuna sehemu walikuwa wanaenda. "Sasa jamani ndio kunifuata usiku nyumbani nataka kulala halafu mbona mmependeza kiasi hicho kulikoni tena.!?" Suzana alibaki kuwatazama wenzake na kuwauliza maana ilionesha walikuwa na safari. "We nae jamani mara hii umesahau wakati tulipanga kwenda santiago club halafu nimepata taarifa kuna band nyingi zitakuwepo, shisha za kumwaga kwahiyo tusichelewe dada fanya haraka twende" "Aaah halafu nilikuwa nimesahau kabisa ok basi sawa nisubiri nijiandae halafu tuelekee huko maana bado muda unaruhusu" Suzana haraka alirudi ndani na bahati nzuri mama yake mkubwa alikuwa amesafiri muda mrefu sana hivyo ikawa kwake huru kufanya chochote. Takribani dakika kumi na tano alizitumia kujiandaa, alipomaliza haraka alitoka na safari ilianza kuelekea santiago club ambapo huko huko Nason na Novan walikuwa wanaenda kufanya jukumu lao la kumuuwa Mr Moses. ******************* Club ilikuwa imefurika, watu kutoka sehemu mbali mbali ya jiji walifika hapo na katika umati huo ndani yake walikuwa marafiki watatu yaani Suzana, Sabina na Sheila, walikuwa wakiangaza huku na kule kutafuta meza nzuri ambayo wangeketi na kupata vinywaji. "Jamani hebu twendeni kuketi kwenye meza ile" Baada ya kuona meza wote kwa pamoja walisogea na kuketi lakini sehemu waliyokaa wao ilikuwa karibu kabisa na sehemu ambayo maongezi ya Mr Moses na tajiri kutoka uturuki yalikuwa yanaendelea na jambo kubwa walikuwa wakiongea kuhusu biashara. Walikuwa hawana ili wala lile na muda huo huo Nason na Novan walifika kama wateja, walitafuta meza na kuketi kisha waliagiza vinywaji ambavyo hawakuvitumia ila waliweka kama urembo huku wakimsomea ramani Mr Moses. Masikioni mwao walikuwa na vibluetooth vidogo ambavyo waliweza kuongea na mkuu wao akiwapa maelekezo nini cha kufanya. "Mkuu tayari tumemuona Mr Moses ila hana ulinzi mkubwa ana vijana wawili tu waliomsimamia pembeni" "Basi muuweni mara moja ila huyo mturuki mumuache maana bosi anamuhitaji kufanya nae biashara, hapo cha kufanya ua huyo Mr Moses ambae ndie kikwazo cha biashara" "Ok sawa" Baada ya mawasiliano hayo Novan na Nason hawakuchelewa walificha nyuso zao kwa mask kisha walipeana signal na kuanza kuwashambulia wale walinzi ili kupata nafasi ya kumuuwa Mr Moses. Risasi mbili zilisikika zilizowaangusha wale walinzi wa Mr Moses chini lakini milio ya risasi hiyo iliwafanya watu kutaharuki na kuanza kukimbia ovyo kutafuta njia ya kutokea humo. Upande wa Mr Moses alijua tayari amekuja kuuwawa maana muda mwingi alikuwa akiwindwa hivyo aliona njia ya kutoka hapo salama ni kumchukua mtu kama ngao ili aweze kukimbia. Alimsogelea kijana wake mmoja aliekuwa chini kisha alichukua bastola na kumvamia binti mmoja aliepita mbele yake ili kumfanya kama ngao na bahati mbaya alikuwa amempata alikua ni Suzana ambae alijikuta akipiga kelele kuomba aachiwe. "We binti tulia mimi siwezi kukuuwa ila nitakufanya kama ngao sasa kama ukileta ubishi nitabomoa kichwa chako" Suzana ilibidi awe mpole kuhofia kufa lakini Nason na Novan walipoona Mr Moses amemtumia mtu kama ngao ilibidi wasogee kwa kujiamini maana walijua hatoweza kufanya chochote. "We mzee hebu acha ujinga sasa unafikiri tukiamua kukuuwa tunashindwa, yaani tunakuuwa wewe na huyo mwanamke kwahiyo muachie huyo binti aende sisi tunataka tudeal na wewe tu" Novan alizungumza huku akisogea zaidi na kumfanya Mr Moses aanze kutetemeka kwa hofu huku kwa Suzana alihisi haja kubwa kumtoka maana mdomo wa bastola ulikuwa kichwani kwake. "Na...nase...nasema asisogee mtu nitaua naombeni mkae mbali, kwanza vueni hizo mask niwaone sura zenu ni wakina nani nyie...!! "Haina haja ya kuvua wewe tunaomba muachie huyo binti aende halafu tutakuacha salama ila kinyume na hapo utakufa" "Sasa nitamshoot risasi kama hamtafanya ninachowaambia" "Ok sawa kuwa mtulivu tutatoa hizi mask lakini umuachie huyo binti" Novan licha ya kuwa muuwaji na mtekaji lakini hakupenda kuona watu wasio na hatia wakifa hivyo ilibidi akubali kuvua mask na kupelekea sura yake kuonekana. "Sasa Novan umefanya nini.!?" "Tulia Nason huyu mzee mbona tutamuuwa wala usijali kwahiyo hapa namzuga tu halafu wewe kaa tayari kumshoot" Mr Moses hakujua kama mipango ilikuwa inapangwa kwa siri, baada ya kuona sura ya Novan alimsukuma Suzana kuelekea alipo Novan kisha alifyatua risasi mbili zilizokuwa zikienda kumpiga Suzana mgongoni lakini Novan aliwahi, alimgeuza Suzana na zile risasi mbili zilipiga mgongoni kwake huku Nason alipata nafasi ya kumshambulia Mr Moses na kumuua.... ITAENDELEA... Story......... PENZI LA MTEKAJI Mkasa...wa...kusisimua Sehemu Ya {02} ILIPOISHIA...... Mr Moses hakujua kama mipango ilikuwa inapangwa kwa siri, baada ya kuona sura ya Novan alimsukuma Suzana kuelekea alipo Novan kisha alifyatua risasi mbili zilizokuwa zikienda kumpiga Suzana mgongoni lakini Novan aliwahi, alimgeuza Suzana na zile risasi mbili zilipiga mgongoni kwake huku Nason alipata nafasi ya kumshambulia Mr Moses na kumuua. ENDELEA NAYO..... Novan alikuwa chini akigugumia kwa maumivu huku damu nyingi sana zikimtoka mgongoni kwake pia upande wa Suzana alikuwa bado mwenye hofu maana alikuwa amenusurika kwenye tundu la sindano pia asingekuwa Novan kukinga risasi basi muda huo angekuwa yeye ndiye anaugulia maumivu ya risasi. "Ka...kaka yangu unaendelaje.!!?" Suzana alisogea mpaka alipo Novan na kumuuliza lakini hakujibiwa kitu, Novan alichukua mask yake na kuirudisha usoni. Wakati huo huo Nason alimchukua na kuondoka nae hawakutaka kabisa kuongea chochote na Suzana walimuacha akiwa mwenye maswali mengi na kujiuliza wale walikuwa ni watu wa aina gani lakini hakupata jibu la kuridhisha akili yake. Wakati Novan na Nason wanaondoka huku nyuma jeshi la polisi likifika baada ya kupata taarifa za uvamizi kwenye club ila walifika na kukuta mashambulizi yamefanyika na kilichobaki ni damu na maiti ya Mr Moses tu. Walitazama pembeni walimuona Suzana ameketi huku akitetemeka kwa hofu, ilibidi wamfuate na kuanza kumuhoji inawezekana wakapata chochote kutoka kwake na wakawajua wahalifu kwa ufupi. "Samahani dada kwanza pole sana kwa kilichotokea hapa najua akili yako haiko sawa kwa sasa lakini nahitaji kujua mawili matatu kwa kilichotokea hapa.?" Askari mmoja wa kike alimfuata Suzana na kuanza kumuuliza maswali lakini Suzana alikuwa mzito kujibu na hata mdomo wake kuufungua aliona kama umefungwa vyuma. "Dada hebu jitahidi japo utueleze machache kuhusu tukio lililotokea hapa lakini ukikaa kimya tutashindwa kufahamu tuanzie wapi tuishie wapi" "Mi...mimi sijui chochote lakini watu waliovaa mask usoni mwao ndio wamefanya hivi lakini kingine sifahamu" "Ok sawa aina shida cctv camera zipo tutaangalia kwahiyo tunaomba uende nyumbani ukapumzike ili akili ikae sawa acha sisi tufanye kazi yetu" Askari ilibidi wamruhusu Suzana kuondoka lakini hata tembea yake ilikuwa kama mtoto mdogo anaejifunza kutembea, basi alitoka mpaka nnje na bahati nzuri kwenye club hiyo kulikuwa na tax nyingi za usafiri zimepaki nnje hivyo aliingia kwenye tax moja wapo na kuomba apelekwe kwake. Wakati hayo yanaendelea Nason alimfikisha Novan kwake na kuanza kumfanyia huduma ya kwanza, alikuwa akimtoa risasi mgongoni pasi na ganzi kisha alimfunga vizuri bandage na kuanza kupiga story zao. "Yaani Novan sasa ulifanya nini pale kumtetea yule binti, mimi nilijua labda utampiga risasi pamoja na Mr Moses na baada yake wewe ndiye umepigwa risasi.!" "Ah sikutaka yule binti afe halafu sisi hatuui watu ovyo ila tunauwa waliokuwa katika target yetu kwahiyo nikaona nimsaidie ila kikubwa mission passed tunatakiwa tukapeleke majibu makao makuu" "Ok sawa haina shida" Novan na Nason walichukuzana hapo na kuelekea makao makuu yao ambapo huko walipokelewa vizuri na taarifa zile zilimfurahisha sana bosi. "Vijana mmefanya kazi kwa weledi mkubwa sana japo kuna makosa mmefanya lakini siku nyingine mabinti kama wale mnaua hakuna kutetea maana unaweza ukajikuta unakufa wewe" "Ok sawa mkuu" Siku hiyo ilifanyika part kwa wahalifu hao lakini Novan hakuweza kuhudhuria maana alikuwa na maumivu makali sana mgongoni hivyo aliomba ruhusu na kurudi kwake kupumzika. Wakati yeye amepumzika kwake na huku Suzana alikuwa amefika kwake muda sana lakini alifikia kupanda kitandani bila kuoga na kuutafuta usingizi ambao ulipeperushwa na mawazo ya tukio lilotokea masaa machache nyuma. "Lakini yule kaka kwanini amenisaidia mimi wakati mimi najua wahalifu hawajali hata mtu akifa kikubwa watimize jukumu lao.!?" "Ila sifikirii kama wahalifu wote watakuwa na roho mbaya, wapo wazuri kama yule kaka ambae ameamua kutoa maisha yake kunisaidia, sasa sijui nitampata wapi angalau nimpe shukurani zangu" Suzana usiku huo ilikuwa ni kuwaza tu kuhusu Novan lakini hakupata majibu ya maswali ila akiwa kwenye msongo wa mawazo simu yake ilianza kuita na aliekuwa anapiga alikuwa ni mama yake mkubwa. Hakutaka kumpuuzia alimpokelea na kumsikiliza alikuwa na mpya gani lakini alimsikia akiongea huku akiwa mwenye hofu sana ambayo ilimfanya Suzana ashindwe kufahamu nini kinaendelea. "Suzana mwanangu upo mzima kweli.!?" "Nipo mzima lakini mama mkubwa kwani shida nini mbona unaonekana ni mtu mwenye hofu sana nini kimekukuta.!?" "Oh asante Mungu uko mzima ila nilikukataza hayo mambo ya club na kutoka usiku ona sasa leo kidogo ufe yaani daah nimevurugwa.!!" "Mama kwani nani kakwambia mimi nilikuwa club pia nilitaka kufa mbona wanakudanganya, mimi sikwenda popote nilikuwa hapa hapa nyumbani nafuatulia mambo ya biashara zangu" "Sawa nifanye mtoto ila siku nyingine sihitaji kabisa utoke usiku na kama unataka kutoka basi uniage na iwe sehemu ya muhimu unaenda lakini kinyume na hapo basi sitakuelewa" "Sawa mama mkubwa nimekuelewa na nikutakie usiku mwema" Suzana ilibidi awe mpole na mdogo kama kidonge lakini alijua lazima taarifa hizo mama yake mkubwa amezipata kutoka kwa rafiki zake, huenda akawa Sabina au Sheila lakini alijua mmoja kati yao atakuwa amepeleka umbea kwa mama yake mkubwa. Ilibidi jambo hilo aliweke kiporo moyoni mwake, alivuta shuka na kuuchapa usingizi huku saa yake ya ukutani ikisoma ni saa nane kasoro usiku. ******************* Siku iliyofuata asubuhi na mapema ilikuwa siku ya Jumapili Novan aliamka mapema sana, licha ya maumivu aliyokuwa nayo mwilini lakini hakujali alifunga safari kuelekea kwenye duka la bidhaa za jumla na kununua bidhaa nyingi kisha alikodi gari na kuzipakia. Ilikuwa ni kawaida yake kila Jumapili kufanya hivyo na hua akinunua mahitaji hayo basi hupeleka katika kanisa kubwa ambalo pia hulea watoto yatima na hata yeye alikulia katika kanisa hilo. Basi alifikisha mahitaji hayo kanisani kisha alikutana na sister Maria ambae alikuwa ni sister mkubwa wa kanisa hilo na huyo ndie aliekuwa akimlea tangu alivyokuwa mdogo. "Novan lakini mbona kila Jumapili ukileta misaada unakuja mwenyewe simuoni mwenzako Nason au hataki kuja kuniona?" "Sijui sister na hata mimi hua namwambia sister Maria amekukumbuka sana anahitaji kukuona lakini anasema tu Jumapili ijayo naenda mara siku ikifika anasema yupo busy basi hata simuelewi" "Sawa kama yupo busy muache najua ipo siku atakuja" "Sawa sister Maria acha mimi niende maana nina harakati nyingi natakiwa nikazifanye basi Mungu akipenda tutaonana Jumapili ijayo na naweza kuja na Nason" Novan aliaga na kusindikizwa mpaka nnje ya kanisa. Kanisa hilo lilikuwa ni kubwa sana na lilikuwa karibu na barabara kuu hivyo wakati huo huo Suzana alikuwa akipita hapo hapo na gari yake ila alipotazama nnje ya kanisa alimuona Novan akizungumza na sister. Alishangaa sana kumuoma Novan hapo kanisani hivyo ilibidi aende mbele kidogo na kugeuza gari yake ili kurudi nyuma lakini akilini mwake bado alikuwa haelewi Novan anafanya nini kwenye kanisa halafu ukizingatia ni muuwaji. "Sasa yule muuwaji anafanya nini pale au ameenda kutubu dhambi zake za jana, hebu kwanza subiri nimfuate nikamuulize vizuri" Suzana alirudisha gari mpaka pale kanisani lakini alimkuta sister amesimama mwenyewe na Novan alikuwa tayari ameondoka. "Samahani sister nilikuwa namuulizia huyu kaka alietoka hapa sasa hivi ameelekea wapi?" "Kuwa mpole binti na karibu, naomba uingie kanisani tuzungumze kisha utafahamu ameelekea wapi usiwe na haraka hata Mungu hapendi" "Ok sawa sister" Suzana ilibidi awe mpole na kuingia kanisani, pia alikuwa akihitaji kujua Novan amefuata nini hapo mbona alimuona akiongea vizuri na sister ilhali alikuwa ni mtu mbaya sana. "Karibu sana binti sijafahamu unaitwa nani lakini najua una maswali mengi kuhusu Novan" "Novan..!?" "Novan ni nani lakini mimi naitwa Suzana Andew" "Jina zuri sana binti ila Novan ni kijana ambae umekuja hapa kumuulizia, yule ni kijana wangu ambae nimemlea tangu akiwa na miaka mitatu mpaka pale unapomuona sasa sifahamu kwanini unamuhitaji halafu unaonekana mwenye shauku sana.!" "Sister mimi nilikuwa namuhitaji yeye ili kumshukuru maana alinisaidia pia kumjua kiundani maisha yake na hapa alikuja kwa lengo gani.!" "Ah Novan ni kijana mpole sana na mwenye kutenda misaada kwa watu wenye uhitaji na hapa alikuja kuleta mahitaji kwaajili ya kuendelea kulea watoto pia anakuwa akifanya hivyo kila Jumapili na kwa miaka mingi sana" "Ahaaa kwahiyo Novan ndio yupo hivyo ila hakuna chochote unachojua zaidi kuhusu yeye.?" "Najua vingi hasa chakula anachopenda, wimbo na hata sehemu anazopenda kwenda kama kwenye sinema na vingine vingi" "Hapana sister namaanisha labda kazi anayofanya au maisha anayoishi?" "Anaishi vizuri tu pia anafanya kazi kwenye supermarket kiufupi hana mambo mengi sana" Sister alijibu kila anachokijua kumuhusu Novan lakini Suzana hakutaka kuongea neno jingine maana yeye anajua kama Novan ni muuwaji na jambo hilo hakutaka kumueleza sister, alimuaga na kiondoka zake. "Inamaana huyu kaka anaitwa Novan, sasa mbona jina zuri halafu ni mkatili sana pia moyo wake mzuri wa kutenda misaada halafu ni jambazi au anafosiwa kufanya haya?" Suzana akiwa kwenye gari alikuwa na maswali mengi sana ya kujiuliza kuhusu Novan pia hakufahamu atampata wapi ili ikiwezekana amjue kiundani zaidi hasa kazi anayofanya na maisha anayoishi. ******************* Majira taratibu yalianza kusogea mpaka inatimu saa sita mchana Suzana alikuwa tayari amefika nyumbaji kwa Sabina na safari yake ilikuwa ikimleta hapo, hakuwa yeye na Sabina tu pia alikuwa Sheila na wote kwa pamoja waliitwa hapo na Suzana. "Suzana mbona umeitisha huu mkusanyiko ghafla halafu unajua leo ni weekend ni siku ya kuenjoy na wapenzi zetu au unatuzuia kusudi ili tusiende kufurahi?" Alizungumza Sabina na kumfanya Suzana amtazame kwa muda kisha alipotezea. "Nyie kweli marafiki, yaani nilifikiri mtauliza nini kilitokea pale baada ya lile tukio ila ndio kwanza mnaanza kuongea shit ok sawa lakini sijapenda tabia yenu kumpigia simu mama mkubwa halafu kumwambia kilichotokea jana" "Lakini Suzana unafikiri tumefanya vibaya, sisi tumefanya ili kukusaidia wewe halafu unaanza kuja kutushutumu kweli wewe huna akili shoga yetu.!!" "Nyie ndio mmekosa akili badala ya kutafuta msaada nikomboke pale ndio kwanza mnakimbilia kusema umbea sijui mpoje ndio maana hamnenepi mnabaki kuwa kama sindano kwaajili ya umbea" Suzana alijikuta akipanic maana jambo walilofanya rafiki zake lilimkera sana. "Suzana naomba utoke kwangu naona sasa umeshindwa kukaa na kuongea vizuri, nenda bhana na najua akili zako zinatokana na kukosa mpenzi kwahiyo ondoka sitaki kukuona" "Ni sawa naondoka ila kesho mjiandae kuja kuchukua barua za kuacha kazi, siwezi kuwa na watu wapuuzi kwenye kampuni yangu" Suzana aliinuka na kuchukua mkoba wake lakini kiukweli alikuwa amechukia sana. "Usitutishe na hivyo vikampuni vyako vya pesa ya mawazo sawa, halafu kama ulikuwa hujui sisi ndio tulikuwa tunatia hasara kwenye kampuni yako, ulikuwa unaishi na virusi bila kujua sasa kaa ukijua" Kama kawaida ya majibizano ya wanawake maneno yalikuwa mengi na matusi ya kila aina lakini mwisho Suzana alitoka nnje, aliwasha gari yake na kuondoka zake huku akiwa mwingi wa hasira sana. Safari yake ilimfikisha supermarket kununua pombe lakini wakati anaingia alipigana kikumbo na mtu lakini yule mtu alimuomba samahani na kuondoka zake. Hakumfahamu alikuwa ni nani ila alipotezea, aliingia ndani na kuchagua pombe alizokuwa anazitaka lakini wakati anataka kulipa, anaingiza mkono kwenye mkoba hakuona chochote. "Mh inamaana sikuja na pesa au nimeziacha kwenye gari.!?" Suzana alihisi kuchanganyikiwa kidogo lakini wakati anakagua mkoba wake vizuri alifika mtu na kumlipia. "Asante sana kaka yangu" Alikuwa ni mwanaume fulani mtanashati ndiye alielipa pesa na mwanaume yule alionekana ni mtu mwenye pesa maana nguo alizovaa zilikuwa za gharama, pete za dhahabu na nyuma alikuwa na walinzi wawili waliokuwa wakimlinda. "Usijali dada mimi naitwa Noel sijui nani mwenzangu.?" "Ah naitwa Suzana" "Oh Suzana ni jina zuri na limekufaa kabisa maana wewe pia ni mzuri na unavutia sana" Mwanaume yule alianza kumtupia sifa kede kede Suzana ambae alijikuta akifurahi sana na kuenjoy lakini Suzana wakati anawatazama wale walinzi wa yule mwanaume alishangaa kumuona Novan na Nason ambao ndio waliokuwa wakimlinda na hii ikamfanya kichwa chake kijae maswali mengi sana.... ITAENDELEA..... SOMA MPAKA MWISHO KWA SH 1000 NJOO WHATSAPP 0682701263

Comments

Popular posts from this blog

Germany: Vice Chancellor Robert Habeck heads to South Korea