STORY PENZI LA MTEKAJI 1 & 2
Story......... PENZI LA MTEKAJI 1......2 Mkasa...wa...kusisimua Sehemu Ya {01} Yapata kama majira ya saa sita mchana, hali ya hewa ilikuwa ya mawingu kuashiria mvua inataka kushuka, jua lilifichwa na mawingu mazito yaliyosindikizwa na upepo mwanana uliomfanya kila mmoja afurahie maana ulikuwa ukivuma taratibu sana. Wakati hali hiyo inaendelea katika ofisi moja ya kampuni ambayo inajishughulisha na maswala ya fashion walionekana mabinti watatu wameketi wakizungumza na mabinti hao walikuwa ni watu wa karibu sana. Walikuwa wakiongea mengi sana lakini kubwa zaidi waligusia swala la mahusiano na kila mmoja alikuwa akisifia mahusiano yake lakini binti mmoja alikuwa kimya na ndie aliekuwa bosi wa kampuni hiyo. Huenda ikawa hana mpenzi au mapenzi yake yalikuwa na mgogoro hilo halikujulikana lakini alionekana kuwa kimya akiwatazama wenzake. "Lakini Suzana we nawe umezidi bosi yaani kila mwanaume anaekutokea na kukutongoza unamkataa sasa sijui unahitaji mwanaume w...
Comments
Post a Comment