
asubuhi anaungana kwenye ibada ya asubuhi, saa 12:00 anaanza kuwaandaa watoto, saa 1:00 anawahudumia wote chakula, saa 1:30 anawapeleka watoto shule kisha anakwenda ofisini. Saa 8 mchana anarudi kuchukua watoto shuleni. Saa 11 jioni anarudi nyumbani, kuanzia saa 12 jioni anaanza kufua na kupika chakula cha jioni. Saa 1:30 usiku anahudumia chakula cha jioni, kisha kuanzia saa 2 hadi saa 3 usiku anashughulikia kazi za shule za watoto. Saa 3:30 usiku anaoga na kuungana na wewe mumewe chumbani, mnaongea na kufurahia ili kukuandaa uwe na hamu ya tendo la ndoa. Wewe mume, ukiwa na kichwa chako kikubwa, unalala kama mfalme.
0 Comments