
. Daktari wake alikuwa amesisitiza kwamba ingawa upasuaji huo haukuwa wa dharura ya haraka, ulikuwa muhimu ili kuondoa tatizo lililokuwa likimtesa kimya kimya kwa muda mrefu. Zarina hakuwahi kuwa na usingizi mzuri kwa siku tatu mfululizo. Kila alipomwangalia Darren usiku, moyo wake ulikuwa unamwambia, asiache kumshika mkono hata sekunde moja. Asubuhi hiyo, nyumba nzima ilikuwa na hali ya wasiwasi. Raveen alikuwa kimya zaidi ya kawaida, akihangaika kuhakikisha kila kitu kiko tayari. Wazazi wa Darren walifika wakawa wametulia huku wakimuomba mtoto wao. Zarina alikuwa na Darren kwenye chumba cha mapumziko walikuwa wamekaa kitandani. Darren amevaa shati jeupe la wagonjwa na suruali
0 Comments