MADAM NIPE KIDOGO BASI 14

Sikutaka kumjibu maana sikuona busara kukaa kujibizana na mama wa mtu, maana ni kama kumvunjia heshima mume wangu… Yule mama alipoona sijibizani nae, akaanza kulia na kusema “ mchawi, sikuwa najua kama huyu mwanamke ni mchawi kiasi hichi, mwanangu tuondoke tusije kumalizwa kama alivyomalizwa kijana wangu, nikashangaa wanaondoka kwa taharuki kisha Yule dada akaniangalia na kusema “ nitahakikisha namtoa mwanangu kwako, maana hatutaki uchawi kwenye familia yetu… Nilishangaa sana ila nikaona ni bora wameondoka maana wakiendelea kukaa pale ni lazima watapoteza amani ya moyo na maisha yangu kwa ujumla… Nikashangaa baada ya kama wiki mbili dada wa kazi anataka kuondoka,

Soma zaidi