
Niliona hiyo ni fursa siku watakazokuwa wanajenga mafundi tutakuwa tunaamka saa 10 za usiku.. Tunawaandalia kiamsha kinywa asubuhi kabla sijaenda chuoni nitakuwa nawapelekeaa nipate na pesa ya nauli za kwendea chuoni🥰🥰🥰... Nilimpatia namba akaondoka....mimi na poppy tulirudi pale mgawahani kwetu tukaosha osha vyombo tukapaweka sawa then tuliondoka kwenda nyumbani.. Siku tunazokuwa mgahawani huwa tunaondoka huko tumekula cha usiku tukifika nyumbani ni kuoga na kukisomea tu.. Siku hiyo baada ya kufika home nilioga nikamaliza nikaanza kujisomea... simu yangu ilianza kuita huo usiku namba ngeni nikapokea.. Sauti kama naijua🤔🤔ni kama ya yule Boss aloomba namba ili awe anaoda chakula.. Helloo... Nikaitikia Helloo..
0 Comments