PAKA WA MAMA KIZIBO  SEHEMU YA PILI

Saa Sita mchana Mwanamtama alikwenda ofisini kwa Bakari. Alipoingia alimkuta Bakari kama alivyomwacha; amekaa, kajiinamia na machozi yakiwa yanamlengalenga. "Bakari, suala lako ni zito sana; na usipoangalia litaharibu hatma yako kabisa. Nilikuwa nikiwaza nikusaidie namna gani. Labda kama utaafiki wewe mwenyewe tujaribu kubahatisha. Hatuwezi kukaa tu kusubiri hawa wahindi wakurarue." Mwanamtama alimsemesha Bakari huku akikaa juu ya Meza baada ya kuhakikisha amefunga komeo la mlango wa ofisi ya Bwana Bakari. Bakari aliposikia maneno hayo akafuta uso na kumwangalia Mwanamtama. Hakusema kitu ila kwa namna alivyomwangalia Mwanamtama ni kama mtu aliyekuwa akisubiri kwa hamu kusikia huo msaada ni wa aina gani.

Soma zaidi