
ENDELEA........ "Naomba aingie kwanza Malkia mdogo Sadia" Sauti ya Mfalme ilisikika. Nilimgeukia Malkia Shamsa nikiwa nimejaa tabasamu. "Nenda wewe, unaonekana kuwa na shida sana ya kuzungumza na Mfalme... Mimi nitakuja kesho " Niliongea kisha ni katega mgongo nisepe. Lakini Malkia Shamsa alinidaka mkono. "Pamoja na yote lakini Mimi ndio Mke wake wa kwanza wa Mfalme. Naheshimika pande zote za hii Nchi" Malkia Shamsa aliongea. "Unaweza kuwa una heshimika lakini ukapoteza nafasi ya kusikilizwa, wewe hapo tayari ushapoteza nafasi ya kusikilizwa " Niliongea kisha ni kaendelea na safari yangu. Nilielekea malangoni kwa Mtabiri Mkuu, nilimkuta akifanya ibaada. Sikutaka kumsumbua nilikaa pembeni
0 Comments