
ENDELEA...... "Mke mwenza .....umesahau wadhifa wangu hata uniite mke mwenza" Malkia Shamsa alionesha hasira zake waziwazi. "Furaha tu ndio imenifanya ni zungumze hivi, nakuomba unisamehe sana " Daktari alijitetea. "Ni dharau, si wewe pekee yako tu...kuna watu sasa hivi nikipita mbele yao wananicheka kimtindo siku ya kesho kutakuwa na msako mkali juu ya watu hao. Sitakuwa na huruma na mtu yoyote yule.... hongera kwa ujauzito. Na hii ni zawadi yako " Malkia Shamsa alizungumza huku akinisogezea boksi . Nilimpa ishara Kijakazi wangu alifungue tuone kilichomo. Moyo wangu ulishtuka baada ya kukutana na panya waliokatwa katwa vipande. "Hivi ndivyo itakuwa endapo
0 Comments