BINTI MIA 04

BINTI MIA Sehemu ya 4 Mwandishi: Chief Hata babangu huwa napenda anavyonukia. Dah, sometimes nampa hata leso yangu aishike ili harufu ibaki. Nikajikuta nasahau matatizo kidogo nikawa napata amani. Basi anavyoongea na ile deep voice yake, basi dah… au basi. Nikabidi ninyanyuke twende tu. Hapo hata nguvu za kumtext Eva nimwambie chochote sina. Ila nawaza mtu mwenyewe chizi, anapenda kucheka. Nawaza leo ndio atanicheka mno. Tukatoka pale. Tukaingia kwenye gari. “Naomba usilie basi, eti sawa?” Akanipa kitambaa chake nikajifuta machozi. “Mna ugomvi na wale ndio nini?” “Tatizo ni masuala tu ya kike. Tulipishana kauli.” “Oky basi usijali. Pia usiwe mnyonge.

Soma zaidi