
MTUNZI SMILE SHINE. WHATSAPP 0688156169. Ukipita wiki moja Amara alikuwa bado anatafuta kazi lakini hakufanikiwa. " Dada tumemaliza wiki na siku zinazidi kwenda kazi bado haujapata? " Kupata kazi hapa mjini ni kazi sana ila sijakata tamaa nimeongea na marafiki zangu watamsaidia . " Bora iwe haraka nimechoka kukaa ndani nataka kutafuta pesa. Baada ya siku mbili kupita Amara alipokea simu kwa rafiki yake na kupewa taarifa kuwakuna sehemu anahitajika msichana wa kazi. Bila kuchelewa Amara alimueleza mdogo wake na kupanga kesho mapema waende kwenye hicho kibarua kipya. Kesho yake mapema Amara na manisha walikuwa njiani wakielekea sehemu husika. Walipofika
0 Comments