
MTUNZI SMILE SHINE WHATSAPP 0688156169 Siku ziliendelea kwenda na Manisha alikuwa akifanya kazi na kulipwa kwa siku . Siku moja Manisha alikuwa amekaa pale barber shop akisoma majarida na kuangalia mitindo ya mavazi. Mara akaona mtu kasimama mbele yake. Alinyanyua macho yake kumuangalia . Alikutana macho kwa macho Ayman . Alimuangalia kwa sekunde kisha akaendelea kufunua lile jarida. " Habari yako . " Salama. Aliitikia maanisha bila hata kumuangalia. " Hivi ndivyo makaribisho wateja? Maanisha alifunga lile jarida na kusema " Ni wewe tena. " Ndio kwani hupendi kuniona hapa? " Sio kwamba sipendi ila mteja wewe ni msumbufu sana.
0 Comments