
Nilimuona kama amechanganyikiwa vile ety anakuja kunioa, atamuoa nani, yaan mimi nikae naeolewa nae ili iweje kwa mfano, mimi siwezi kuolewa na mwanaume kama Yule maana kwanza amesababisha sijamaliza mtohana wangu wa mwisho na pili ameniingilia kimwili bila ridhaa yangu, nilijua hata iweje siwez kuolewa nae maana alizidisha chuki moyoni mwangu mara baada ya kuniingilia kimwili, ila sikutaka kumjibu manaa nazijua hasira zangu, yaan nikishakuwa na hasira tu mdomo unakuwaga wazi, naweza kusema kitu ambacho sikutegemea kabisa kukisema .... Akaniangalia maana alijua kuwa nina hasira nae zaidi, yaan kasababisha nisifanye mtihan na kunibaka kanibaka, akaniangalia kwa kama dakika mbili hivi
0 Comments