
By Babie LOve Yani ndo kwanza nilikuwa nimeingia ndoani na mabalaa nayo yakaanza siku hiyohiyo 🤣nilikuwa bize nasubiria mume atoke kuoga tuingie kwenye ulimwengu wa maha😁ba lakini mambo yalibadilika.. Msg iliyotoka kwa shemeji yangu Morgan iliandikwa hivi.."huyu mwanamke analia sana amegoma kabisa kula chakula na hali yake inazidi kuniogopesha.." "Tafuta upenyo hata wa dakika 15 tu uje uongee nae at least ale hata chakula naogopa anaweza akatufi a please Bro jitahidi usipuuzie" Wawili hawa inaonekana walikuwa wanachart tangu tukiwa ukumbini ni vile tu sikuwa naijua password ya simu ya Bill ningekagua nijue ni mwanamke yupi aliekuwa anazungumziwa.. Niliwaza cha kufanya
0 Comments