
Niliisoma meseji iliyoingia kwenye simu ya jimama huyo mara mbili mbili huku macho yakiwa yamenitoka na mikono ikianza kutetemeka, "Huyu mama anameza vidonge gani tena siyo vile vya naniliu kweli, kama vile basi nimekwisha, kwanini sikuwaza kutumia kinga mimi?" Nilijikuna kichwa na wakati huo huo jimama hilo lilijigeuza taratibu nikarudisha simu yake haraka kabla hajagundua kuwa nimechungulia. "Uuuwiii kiuno changu mie" alilalamika "Pole" "Za asubuhi" "Salama" niliitikia kama sitaki "Vipi mbona umesimama tu, saa ngapi kwani saa hizi?" "Saa moja" nilimjibu na wakati huo huo simu yake iliita tena akapokea "Shikamoo mama" "Marahaba mbona asubuhi asubuhi?" "mama hivi umemeza vidonge
0 Comments