
"Mama shikamoo" nilimsalimia huku nikijikuna kichwa, "Sitaki shikamoo yako, nakuuliza umemfanya nini Getu wangu jana wewe kijana, eeh?" Mama huyo alikuwa mkali na wapita njia kama kawaida hawataki kupitwa na jambo wakaanza kujongea jongea kutaka kujua kulikoni kama ilivyo kawaida ya Waswahili "Lakini mama mimi sijamfanya binti yako kitu chochote kile" "Kwa hiyo mimi muongo eti wewe kijana?" "Hapana sijasema wewe ni muongo mama yangu ila.." "Ila nini?" "Naomba basi tuongelee pembeni si unaona hapa tunajaza watu" "Getu, twende" alimshika mkono binti yake huyo mwenye matatizo ya akili akimvuta twende pembeni kama nilivyomuomba, tuzungumze, tukazunguka nyuma ya nyumba moja ili
0 Comments