
Kula Chuma hichoo👇🔥 "Mama Getu, mama Getu mpo humo ndani?" Mlango uliendelea kugongwa, "Bonny nenda chumbani kajifiche wasije wakakuona hapa" aliniambia nami nikatoka na kurudi chumbani haraka lakini sikurudi chumbani kwake, ilibidi niingie kwenye chumba kingine isije ikawa ni mumewe akaingia chumbani kwao akanikuta likawa balaa jingine, nilipojificha nikachungulia kidogo kwenye uwazi wa mlangoni na kusikiliza kitakachoendelea. Nilimwona mama Getu akihangaika hangaika kuweka vitu vizuri sebuleni kama mito na kufuta futa masofa huku akijinusa nusa yeye mwenyewe kama ana jasho, akafuta futa chini kisha akaenda kufungua mlango, nikaona wanaume wawili wenye suti na mwanamke mmoja wakiingia ndani sebuleni lakini hakuwapeleka
0 Comments