
ENDELEA.......... "Baba unatafuta nini hapa " Nilishtuka mno baada ya kumuona Baba yangu. Unajua simsemi vibaya lakini kama asingekuwa na familia angekuwa kibaka mkubwa aliyeshindikana.....kuna hadi Mimi huwa ananiibia. "Yaya wa Mtoto wa Mfalme kwa nyota ipi uliyonayo .....hebu naomba ujielezee haraka kwa sababu nimekutafuta sana huko mtaani hadi magerezani lakini sikuambulia kitu" Baba aliongea. Vile mwenyewe ni mapengo sasa mtoto alianza kulia. "Hebu nifuate haraka " Nilimuambia kisha ni kamuingiza chumbani kwangu. Sikuwa na namna zaidi ya kusimulia mambo yalivyokuwa. Ile Baba anataka kufungua mdomo wake kuzungumza mlango uligongwa. Ilinilazimu kumuweka chini ya uvungu. "Karibu mheshimiwa Malkia " Niliongea
0 Comments