
Dada umeamkaje "nimeamka salama mdogo wangu vipi mbona Asubuhi asubuhi leo" aaah naenda kikundi mala moja kuchagua viwaro kidogo si unajua muda mlefu umepita sija daka vitu vipya "ila dogo bwana haya nenda leo unaenda peke yako pacha wako muddy si mwoni?" Na mwachaje dada yupo njiani tuta kutana mjini huko huko "haya dogo vipi chai niwa wekee ?" ndio dada weka, Ngoja nikavizie bajaji pale "haya dogo" nilisogea hadi mzambalauni kuvizia bajaji zinazo toka nane nane haikupita muda bajaji ilisimama mbele yangu oya mjini jelo hili hapa "panda twende mjomba" fasta nikazama kwenye bajaji mwendo haikuchukua muda kuingia mjini
0 Comments