
Yule baba alikuwa anaongea kwa upole na kwa busara ya hali ya juu, yaan maneno yake yote tuliyaelewa vyema kabisa, nabil akamuangalia baba yake wa mchongo kisha akasema “ nampenda sana mama na nakupenda sana wewe, ila naomba nikawaone hata wazaz wangu, na nitaongea nao, na ninakuhakikishia hawatakuwa na shida kabisa kwa mimi kuwa kijana wenu ila angalau tu wajue kuwa nipo hai, kwa sababu nimesikia mama yangu hajawah kuacha kulia kuanzia aliponipoteza… Yule baba alituelewa, na tukalala, na kesho yake nabil aliamka na kupika chakula ambacho alikuwa anakipenda sana mama yake, na mama yake akafurah sana, kisha wakawa wanataniana
0 Comments