
“Ndeana, umeniuliza maswali kwanini wewe, kwanini nakupenda sana wewe. Nakupenda kwasababu Nakupenda sana. Nakupenda kwasababu unastahili kupendwa, Unastahili heshima, Unastahili upendo wote hapa duniani, Ndeana kila kitu kizuri ni kwaajili yako. Umefanya mambo makubwa sana kwenye maisha yangu. Pengine kikawaida wewe hauwezi kujua wala kutambua hilo. Ila niamini mimi, ipo siku nitakuelezea kitu umefanya katika maisha yangu, Ndeana wangu, mtoto mzuri, Ndeana mwanamke mzuri sana. Nimekuleta hapa nataka ufurahi, nataka ufurahi zaidi ya wanawake wengine wote wanaoletwa hapa na wapenzi wao, wanaume zao. Kwako iwe tofauti, sawa sunshine.”. Akacheka kidogo kufanya nione tena meno yake mazuri na meupe namna yamepangika
0 Comments