
Mvua kubwa ilikuwa ikinyesha usiku huo , barabara ilikuwa na unyevu unyevu uliopambwa kwa taa hafifu za barabarani alionekana msichana mmoja mrembo aliyevalia gauni lake la kitenge refu mpaka nchini akitembea kwenye mvua bila kujali chochote mwili wake wote ulikuwa umelowa sana na USO wake ulionekana kuwa na huzuni ,watu waligeuka kumuangalia ni wazi walimshangaa sana kwani hakuwa na kitu chochote Cha kumkinga na mvua Yani mwamvuli Dakika chache tu zilitosha yeye kufika nyumbani kwao " Winnie mjukuu wangu kwani hii mvua huioni utapata homa ungechukua hata bajaji " alisema bibi mmoja huku akimfunika yule msichana kwa kutumia kitenge chake
0 Comments