
Naitwa Magreth (Mage) kumbuka nilikuwa kidato cha pili kipindi hicho najiandaa na mitihani ya Taifa katika shule ya sekondari Tambaza, ilikuwa jioni ya saa kumi na mbili ikielekea saa moja giza likiwa limeshaanza kuingia tayari, ingawa huwa ninatoka mapema saa tisa lakini siku hiyo tulichelewa kwa ajili ya watu wa mazingira waliokuwa wametutembelea shuleni kwetu. Kichwani sikuwa haba, nilikuwa nina akili za darasani na ndiyo maana nikachaguliwa kujiunga na shule hiyo maarufu ya Wasichana pekee ambayo ilikuwa miongoni mwa shule kumi bora zinazochukua watu wanaofaulu kwa maksi za juu kipindi hicho, zikiwemo Jangwani, Kisutu Girls, Zanaki na zingine za wanaume
0 Comments