
“Kubam!” mlio wa mlango kubamizwa kwa nguvu ulisikika. “Shoga hebu nipe huo ubuyu wa moto kabla haujapoa,” Esta alisema hivyo kwa shauku ya umbea, ndiye aliyebamiza mlango pindi alipoingia ndani ya chumba “Kiherehere changu chote cha mapenzi kimeniishia,” alisema Muna akiinamisha kichwa chake chini “Kiherehere? Hebu jifunue nielewe basi,” “Ni Hilali,” “Hilali! Kafanya nini?” “Acha tu, sijategemea kwakweli, nahisi kuchanganyikiwa,” “Kabla hujachanganyikiwa niambie kwanza, maana ukishachanganyikiwa sitoweza kupata ubuyu wangu wa moto, ujue simu yako ndiyo iliyoniharakisha!” “Hivi wanaume wa siku hizi wana shetani gani?” “Na wewe usinichanganye sasa, nikichanganyikiwa sitausikia huo umbea,” “Halafu uniletee vituko, mwenzako niko njia panda sielewi hata nifanye nini?” “Hapo
0 Comments