
Nilifanya kama, alivyonielekeza mme wangu, Najma aliletwa mpaka tunapoishi, akae hapo, na mwanae mimi kama siwezi kukaa nae basi niondoke,aliletwa na mama mkwe, mimi ata sikujibu chochote, nilikuwa nataka kutoka nikaghaili, nilikuwa nishampeleka mtoto shule, ikabidi niingie chumbani nikajifungia, nakumpigia Naseer nikamuomba aje kidogo nyumbani kama ananafasi, akapata hofu kuna tatizo? Nikajibu hapana nilikuwa nimekumiss tu... Alishangaa, akasema unauhakika nikajibu ndio, akasema anakuja, kweli hakukawia akawa amefika, alishangaa kumkuta Najma, alimtizama kwa jicho kari, Najma aliinuka ili ampokee, Naseer aligoma akamkwepa nakukimbia kuja chumbani uku ananiita, nilifungua mlango, akawa ameingia,tukafunga, akashusha pumzi uku kanuna ehee hiki nini? Ilibidi nianze kumuelezea
0 Comments