Chombezo : Jamani Kaka Cheni … Ndiyo Nini Sasa?! Sehemu Ya- 2 Nilimwona kaka Cheni akishtuka sana. Hata mimi nilishtuka kwani nilijua baba

Chombezo : Jamani Kaka Cheni … Ndiyo Nini Sasa?!  Sehemu Ya- 2   Nilimwona kaka Cheni akishtuka sana. Hata mimi nilishtuka kwani nilijua baba

ameshakwenda kazini kwake, kumbe alikuwepo bwana. “Shikamoo baba,” kaka Cheni aliamkia huku wasiwasi wake ukiwa umegundulika na baba. “Marhaba.” Baba yetu alikuwa na tabia hiyo ya ajabu, ukimwamkia akiitikia hana cha kusema umeamkaje wala habari za leo! Hilo hata mama alikuwa akimshangaa. Mwenyewe msimamo wake ni kwamba, kumuuliza aliyekuamkia shikamoo umeamkaje ni kupoteza sauti kwani angekuwa ameamka vibaya asingeamkia shikamoo angeeleza ugonjwa wake au tatizo lake. Nilianza kutetemeka mimi badala ya kaka Cheni licha ya kwamba naye kaka Cheni hakuwa sawasawa hata kidogo. Ishu ilikuwa lile jimwanamke kutoka chooni. Kwani ilikuwa lazima kaka Cheni amfuate akamstopishe au aache atoke mwenyewe

Soma zaidi

Post a Comment

0 Comments