
Chombezo : IMEANDIKWA NA : MAZUNDURU ATHUMANI Sijui nini kiliendelea, nilipitiwa na usingizi moja kwa moja na kuja kushtuka saa kumi usiku nikiwa napitisha kumbukumbu kichwani, nikakumbuka mara ya mwisho ilikuaje. Nikakumbuka nilifikia sehemu moja na kaka Cheni na mwanamke wake, nikakasirika sana. *** Asubuhi ilifika, kulikucha, nikatoka kufanya kazi za ndani uani huku nikiwa nalenga kuona kama yule mwanamke wa kaka Cheni aliondoka au alilala palepale. Nilifanya kazi kwa umakini wa macho. Muda mwingi nilikuwa nakazia macho mlangoni kwa kaka Cheni. Saa moja, kaka Cheni alifungua mlango wake. Akatoka yeye akiwa amevaa bukta nyeusi tu, juu alikuwa kifua wazi.
0 Comments