
"Unaniacha niondoke au niyakate haya makendelu yako?" Hapo sasa mama Amina alizamisha mkono mfukoni kisha alichomoa kisu! ***** Amina alikaa sana kule nje akimsubiri mama yake. Dakika nyingi zilipita pasipo mama yake kuonekana. Hata hivyo hakuwa na shaka, alihisi labda mama yake anaumwa tumbo ndio maana kachelewa kutoka chooni. Binti wa watu aliendelea kusubiri. "Ila mbona anachelewa sana? Hata kama anaumwa, ndo ugonjwa gani huo?" Amina aliwaza. Alisubiri sana ila mwisho aliingiwa na wasiwasi, aliona ni bora akapate uhakika wa mama yake. Alilipiga hatua kuelekea chooni, alifungua choo kimoja badala ya kingine akimtafuta mama yake. "Mamaaaa....mamaaa...mama upo wapi?" Amina aliita.
0 Comments