
Mtu akitaja neno Zanzibar, kinachotakiwa kuja kichwani kwako haraka ni harufu ya karafuu, mandhari ya mji mkongwe na fukwe nzuri, ndiyo; hiyo ni kwa wanaoijua Zanzibar vilivyo kuanzia Unguja; Pemba na visiwa vyake. Lakini kwa wengi wetu ukitajiwa Zanzibar, kichwa kitavuta taswira za fukwe safi, mitumbwi, minazi, wapemba na mavazi yao na ile lafudhi yao maridhawa ya Kiswahili. Hiyo ni kwao hao watu wengine, lakini si kwa mzee Damian Shirima, yeye kwake neno Zanzibar lilimtia ashki na midadi kumpanda maana taswira iliyomjia ni ya Naifathy binti wa Kipemba anayekutana naye akiwa Mangi huko Zanzibar miaka mingi mno iliyopita. Nini alichofanyiwa
0 Comments