
Bwana muddy alifanikiwa kutoka jela huku akiwa amenawiri kwani ilifika kipindi akazoea maisha ya mule ndani mwili wake uli ongezeka alifuga na mzuzu wa kutosha juu alikuwa na kipara kilicho kolea mafuta na sasa alikuwa nje ya geti kuu la gereza la butimba lililopo mkoani Mwanza Maisha yalikuwa yame badirika sana jiji la mwanza lilizidi kupendeza majengo makubwa yalizidi kuongezeka baada ya kutoka alikuja kupokelewa na dada yake mkubwa ambae ni mama ashura alisikitika sana baada ya kupewa taarifa za mke wake kuwa alisha olewa na mzungu na kwa sasa yupo nje ya nchi mali zake zote zilikiwa zimesha taifishwa
0 Comments