
Dokta Temba alishangaa sana na kubaki akijiuliza usiku huo aliona nini mpaka aogope kusema akihofia mdogo wake kufa, ila mimi na wewe msomaji tunajua kabisa kuwa aliwaona wachawi japo anaogopa sana kusema akihofia uhai wa mdogo wake. Basi walirudi nyumbani na kumkuta mama yao akiwa amemaliza kuwaandalia chakula, walikula na wakatambulishana kwa kina, ila dokta Temba akawashtaki akina Dorini eti wamempatia life story yao ya kusikitisha ila ikaishia njiani, palepale mama akaomba na yeye ahadithiwe kisa-mkasa hicho mwanzo mpaka mwisho. Dorini akaanza kusimulia yote ila akakomea kubakwa, habari za wachawi hakuthubutu kabisa hata kudokeza. Mama yake alishtuka kisha akasema “We
0 Comments