
DADA WA KAZI KELVIN MLOWE EPISODE 3 Kulipopambazuka, mvua ilikuwa imeacha manyunyu yake kwenye majani na paa za nyumba. Hewa ilikuwa tulivu, lakini ndani ya moyo wa Neema bado kulikuwa na vuguvugu la maumivu, mchanganyiko wa mshangao na hasira ya usiku uliopita. Alimwangalia mumewe Baraka akiwa amelala, uso wake mtulivu kama mtoto, bila hata kujua namna moyo wa mkewe unavyochacha. " Kweli kwa huyu mwanaume navomjua anavopenda kula tunda, atakuwa hajala tunda la mfanyakazi mmmmmh hapana lazima kunakitu wananificha hawa ila nitajua" Lakini mbona lile kufuri lake lilikuwa pembeni na mume wangu alikuja jikoni kifua wazi ina maana hakula kweli
0 Comments