
Kutoka mliyayoyo hadi msindo mwendo ulikuwa ni mdogo mdogo kulingana na barabara kuwa yenye mashimo mengi na udongo mwekundu ngunja ilichukua kama dakika 20 hivi tukawa tayali tumeingia ardhi ya Msindo ,Dereva alipenda sana maandhali ya Msindo na akawa anauliza hapa ndio mshindo nilitabasamu na kumwambia sio mshindo ni Msindo oooh sawa gari ilikuwa inatembea mwendo mdogo sana na hatimae tukaipita kichangani na kuanza kuipata pacha nne tulienda mwendo mdogo sana huku tukiwaona wa mama wamebeba kuni wengine ndoo kichwani mbele kidogo kulikuwa na watu wengi pembeni nika mwambia dereva pitia njia hii nyumba zile ndo kwenye msiba basi alifuata
0 Comments