
Baba mkwe alikuwa akisikiliza maongezi yetu pasipo kuchangia kitu, mda wa kulala ulipofika mimi na Nasir tulielekea chumbani huku wazazi wake wakienda kulala kwenye chumba kingine. Bahati mbaya nyumba yetu ilikuwa ndogo na ilikuwa na vyumba viwili tu, mbaya zaidi vyote vilipakana kiukaribu zaidi. Siku hiyo Nasir hakuwa na hamu ya kufanya mapenzi hivyo mwenzangu alianza kusinzia wakati huo mimi nikiutafuta usingizi, kwenye chumba walichokuwa wamelala wakwe zangu nilisikia mama mkwe akipiga kelele. "Woi woi woi woi woi" "Mmmmh kinaendelea nini huko!?" nilijiuliza baada ya kuisikia sauti ya mama mkwe wangu hivyo niliamua kumuamsha Nasir. "Nasir amka!" "Nini Fatuma mimi
0 Comments