
Siku moja Shahid alikuwa anatoka kwenye suparmaket moja akiwa anaenda kwenye gari lake alimkuta Shania akiwa amejibanzaa sehemu akiwa analia na baadhi ya watoto wakiwa wamesimama wakiwa wanamuangalia. Shahidi alisogea mpaka karibu kuangalia Alimkuta Shania analia Shania unalia nini? Shania hakujibu aliendelea kulia huku akijikinga mwilini mpaka zile sehemu nyeupe za mwili wake zilikuwa nyekundu. Kwa wazo la haraka Shahid alihisi huenda amekula kitu ambacho kimempa aleji lakini mtoto mmoja akasema. Yule mtoto kammwagia upupu. Upupu? Shahidi aliuliza kisha akachuchumaa. kumuangalia vizuri, Shania aliendelea kujikuna mpaka ngozi ilikuwa nyekundu Shahid aliwaza atamsaidiaje lakini hakupata jibu. Mungu wangu nitamsaidia je sasa?
0 Comments