Kwa hiyo umekubali kuzima matumaini makubwa ya nyumbani kwenu juu yako ?

Kwa hiyo umekubali kuzima matumaini makubwa ya nyumbani kwenu juu yako ?

Umekubali na kunyoosha mikono juu kwamba , safari yako imeishia hapo ? Tuseme zile ndoto zako , zitabakia kuwa hadithi ya kufikirika kwa upande wako ? Kwa hiyo na wewe pia umeshindwa kuwaheshimisha wazazi wako ? Tukikuuliza kwa nini , unajibu kwa sababu ya changamoto kubwa... Sikia hustler hakuna changamoto kubwa , mbele ya ndoto zako kubwa... Matumaini ya wazazi nyumbani ni makubwa , kuliko changamoto unazokutana nazo... Unakubali kufa huku ukiwa hai , nani sasa atalibutua kopo linaloitwa umaskini nyumbani kwenu... Sababu zote , zinakataa wewe kukata tamaa , twenzetu tukajaribu na leo, labda itakuwa tofauti na jana... LECTURE...

Soma zaidi

Post a Comment

0 Comments