
_________________________________ Kumtizama hivi, nilishtuka ilikuwa ni ghafra sana kuwaona mbele yangu nilijua hata wameshaondoka, alikuwa ni yule dereva wake wa siku zote, anaemleta Amina shule, aliomba tuongozane wote, familia imeomba nikajumuike nao kwa mlo wa jioni, yaani matajiri hata hawajaniandaa khaa, nikaomba nikajiandae kwanza, alikubali nilifunga… Nikaenda kujimwagia nikapiga pamba zangu, Nina mwili wa nguo yaani hata nivae nini lazima nitapendeza, nilivaa kawaida ila mwenyewe nilijiona kabisa nimevutia.. Nilitoka nikapanda hao kwao Amina , muda huo nimeshatoa taarifa kwa ndugu nikitekwa wajue pakuanzia nilituma plate no za gari,na maelezo mafupi kabla yakutoka, Kisha hao tukalianzisha kwenda huko kwao Amina binti
0 Comments