
mbali na frank, nikajikuta nilishindwa ata kumkumbatia na kwa sauti ya utulivu nikazungumza. "Unaniumiza" Frank akaniachia kwa haraka kisha akaniuliza "Oooooh pole kwani Bado unaumwa au ?" "Niko Sawa" Nilijibu kisha nikasogelea meza yangu na kukaa na kuanza kupitia kazi zangu "Naona Sina kazi Mpya na Leo ni jumatatu" Nilimwambia frank. "Aaah usijali kazi zako zote za Leo nilikufanyia Jana na Leo jioni nitafikisha sehemu husika" Alijibu frank Tena kwa kunichangamkia sana, Yaani frank alikuwa ni wa tofauti sana sio frank. Yule kauzu, Yaani alikuwa ni frank Mpya kabisa sio Yule ambaye ata salamu yake ilikuwa ni shida kubwa sana
0 Comments