
Kwa majina naitwa Miranda,ni mtoto wa pili katika familia ya watoto watatu. Wakwanza akiwa kakangu Collins nafata mie kisha anafata mdogo wangu Veronica. Familia yetu nilikua ya kawaida tu pesa iliopo ni ya kubadilishana mboga tu. Baba na mama yangu walikua ni watu wanaogombana sana na hatukuwagi jua sababu haswa ni nini ya ugomvi wao wa mara kwa mara ila tulikua tunaskia wanagombezana wakiwa chumbani na kupigana huko huko chumbani kwao. Kaka yangu alikua anachukia sana tabia hio maana yeye alikua na uelewa kidogo kipindi hiko kuliko sisi ambao tulikua wadogo. Nikiwa na miaka 16 hapo nimemaliza kidato cha nne
0 Comments