MUCHAS GRACIAS SOFI MARTINEZ POR LA HISTORIA ❤️❤️ Wakati dunia

MUCHAS GRACIAS SOFI MARTINEZ POR LA HISTORIA ❤️❤️ Wakati dunia

ikiwa kwenye duwazo la kiwango bora cha Lionel Messi siku ile ya Disemba 13, 2022 kwenye nusu fainali ya Kombe la Dunia dhidi ya Croatia…! Bado kulikuwa hakuna majibu sahihi ya kwa nini Messi anafanya vile akiwa na miaka 35 dhidi ya mlinzi imara kama Joško Gvardiol✍️ Wakati ambao timu imemaliza mchezo kama kawaida…! Waandishi walikuwa kwenye eneo huru la mahojiano (Mixed Zone) na bahati ikawa kwa mdada Sofi Martinez ambaye Microphone yake ilikuwa mbele ya Messi na akauliza maswali yake mafupi tu. Bahati huwa haiji mara 2. Huenda asingepata nafasi kama hiyo tena na akaamua kumaliza kila alichokusudia kusema…!

Soma zaidi

Post a Comment

0 Comments