
Siku ya pili palipo kucha, Leila aliamka mapema sana akiwa ana smile vibaya mno. Hela aliyokuwa ameipata usiku ule mmoja kwa kudansi hakutegemea kama angeipata kiulaini tena kwa dakika 10 za kutingisha nyama nyama zake😋. Kwa haraka akavaa nguo zake, akaziweka pesa vizuri kwenye pochi kisha akaondoka kuelekea hospitali. Alipofika wodini, aliwakuta wauguzi wakiandaa kifaa cha dialysis. Daktari alipomuona Leila alimwita pembeni na kusema, “Kama mmeshapata kiasi cha awali, tunaweza kuanza matibabu sasa hivi” Leila alifungua pochi yake akatoa kiasi chote cha pesa na kumpa “Hii hapa, daktari. Tafadhali mfanyie lolote linalohitajika. Sitaki kumwona Lulu akiteseka tena” “Asante umeleta hela
0 Comments