
Nilichoka. Sio kuchoka kwa kulala, bali kuchoka kwa maisha kunipiga makofi kila siku. Kazi ni nyingi, mshahara ni mwembamba, nguvu zimekataa kushirikiana na ndoto zangu. Nikajiambia: “James, huwezi kuendelea hivi. Tafuta msaada.” Ndipo wazo likanijia kichwani kama umeme wa ghafla: NINUNUE ROBOTI! Niliona matangazo yakisema: “Roboti la kisasa – linafanya kazi zote za nyumbani, lina akili bandia, halichoki.” Nikafurahi nikasema: “Hata mimi akili yangu siku hizi ni bandia, tutashirikiana.” Nikauza vitu kadhaa, nikakata matumizi, nikakopa kidogo, nikafanikiwa kulinunua. Roboti lilikuwa zuri kupita maelezo . Macho yanawaka, linatabasamu, sauti laini kama mtangazaji wa redio. Muuzaji akaniambia kwa kujiamini: “Ukilinunua hili, maisha
0 Comments