
________________________________________* *SEHEMU YA SITA* Kuna tabia kwenye maisha yangu nilijiapiza sitakaa nifanye. 1. Kutoa mimba. 2. Kwenda kwa waganga na 3.Kuchepuka. ni Tabia ambazo nimeshuhudia madhara ya moja kwa moja kwa wanaofanya hivyo. Hivyo nilijiapiza kamwe sitathubutu maishani mwangu kuchepuka. Haijalishi nitapitia changamoto gani. Nimeishi ndoa ya mateso sana. Lakini nachepukaje?mume kahama chumba. Kamjengea mdogo wangu nyumba na ni mke wake. Wanaishi maisha ya starehe sana. Sasa si aniache tu wakishi na mdogo wangu?mbona ananiganda?nawaza. Lulu wangu, mbona umehama kabisa kimawazo?Machozi yanaana kunichuruzika. Filex nisikilize, hakuna kitu naogopa kama kuchepuka. Naogopa sana. Sijwahi na sitamani kufanya hivyo kabisa. Niliendelea kulia.
0 Comments