
Klabu ya Simba SC imekamilisha usajili wa kiungo fundi kutoka Senegal Alassane Maodo Kanté (24) akitokea klabu ya CA Bizertin ya Tunisia. Kanté anasifika kwa uwezo mkubwa wa kukaba, kupora mipira, na kuchezesha timu katikati ya uwanja akiwa kama kiungo mkabaji (defensive midfielder). Mchezaji huyo aliyewahi pia kupita katika klabu ya Teungueth FC ya kwao Senegal, ni sehemu ya kikosi cha taifa cha Senegal kilichoshiriki COSAFA Cup mwaka 2022. Ni kijana mwenye nguvu, nidhamu na uwezo wa kupiga pasi ndefu na fupi kwa usahihi wa hali ya juu. Kanté anatarajiwa kuongeza nguvu mpya kwenye safu ya kiungo ya Simba kuelekea
0 Comments